Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu itaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli unaimarishwa kwa kutenga fedha kila mwaka ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo ya ndani na nje ya Tanzania inayosafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza katika Kikao cha Utatu kilichojumuisha Balozi wa China, Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Tanzania na Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Serikali ya Zambia kilichofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma, Waziri Mbarawa amesema kuimarisha kwa usafiri wa reli wa nchini hususani Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kutapunguza changamoto.