29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaweka mikakati kuwa kinara uzalishaji mawese

Na Editha Karlo -Kigoma

WAZIRI Mkuu, Kasim Majaliwa, amesema safari ya Tanzania kuelekea kujitegemea katika uzalishaji wa mafuta ya mawese imeanza na itaondoa hali ya sasa ya Serikali kutumia Sh bilioni 445  kwa kununua mafuta hayo nje ya nchi.

Majaliwa alisema hayo jana wakati akizindua upandaji wa michikichi kwenye mashamba ya wakulima mkoani hapa na kusema sasa Tanzania inaanza kuandika historia ya  kuingia kwenye takwimu za kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta ya mawese barani Afrika.

Akinduzia mpango huo kwenye Gereza la Kwitanga wilaya ya Kigoma na Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JkT) Burombola kikosi Cha 821 wilaya ya Uvinza, alisema Serikali imewekeza nguvu za kutosha kutekeleza mpango huo na kwamba miaka mitano ijayo Tanzania itakuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa mafuta ya mawese barani Afrika.

Aliagiza kutambuliwa kwa wakulima wanaolima na wanaotaka kulima michikichi ili wapewe mbegu bure, kuweka mazingira ya wataalam wa ugani kuwafikia, kuratibu upatikaji wa teknolojia na mikopo kwa wote wanaolima michikichi.

Alisema utekelezaji wa mpango huo unatokana na msukumo mkubwa uliopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo kila wakati viongozi wa chama wamekuwa wakiomba taarifa ya utekelezaji kwenye kilimo ikiwemo kilimo cha michikichi.

Sambamba na hilo alizita kambi ya JKT Burombola na Gereza la Kwitanga kusimamia kwa karibu mpango wa Serikali kwa taasisi hizo za majeshi kusimamia kwa karibu utekekezaji wa kilimo Cha mashamba makubwa ya michikici na uzalishaji mkubwa wa mafuta ya mawese.

Awali Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema Serikali imeimarisha kituo cha utafiti wa michikichi Kihinga ambapo wataalam 13 wamepelekwa kwenye kituo hicho wakiwemo watafiti tisa waliobobea kwenye kilimo cha michikichi ambao watawezesha kufikia lengo la kuzalisha miche milioni tano miaka mitatu ijayo 

Mgumba alisema lengo hilo linaenda sambamba na lengo la uzalishaji wa miche milioni 15 kila mwaka kwenye mikoa inayolima michikichi nchini na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta ya Mawese nchini.

Naye Waziri wa elimu, sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, aliipongeza Serikali kwa utekelezaji wa mpango wa kilimo cha michikichi mkoani Kigoma kwani kimeupa heshima kubwa mkoa huo lakini utaufanya mkoa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles