31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RAIYMEK DE LA ROSE: ‘Pacha’ wa Abdukiba anayekimbiza Marekani

 CHRISTOPHER MSEKENA 

KUTOKA Spokane, Washington huko Marekani, Aimer Wabulassa a.k.a Raiymek De La Rose ni miongoni mwa vijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaofanya vyema kwenye muziki. 

Swaggaz wiki hii tumefanya mahojiano maalum na msanii huyo ambaye anatamba na ngoma yake, Washa aliyoiachia hivi karibuni kwenye mitandao mbalimbali ya muziki duniani. 

Swaggaz: Raiymek De la Rose ni nani na lini ulianza kufanya sanaa yako? 

Raiymek: Nimetokea Goma, Kongo DRC na nilianza muziki kanisani mwaka 2001 ila kujiweka zaidi kwenye sanaa nilianza kwa kusikiliza muziki wa Hip hop mwaka 2005 na hapo nikajua nina kipaji na nyota kutoka kwa Mungu na nikafanikiwa kupata sponsa mwaka 2012-2016. 

Swaggaz: Ukiwa kama kijana wa Kiafrika unapata changamoto gani kufanya muziki wako Marekani? 

Raiymek: Zipo nyingi ila ya kwanza ni menejimenti sababu unapotaka kupiga shoo unahitaji vibali vya serikali sasa hiyo huwezi kama huna menejimenti. 

Changamoto nyingine ni mwitikio mdogo wa muziki wa Afrika hasa huu unaotumia lugha ya Kiswahili, mimi nimeshatuma sampo za ngoma zangu kwenye lebo kubwa hapa Marekani lakini sipati majibu na mara ya mwisho waliniambia hawaelewi lugha. 

Nyingine ni haki miliki za muziki wangu, unapata shoo unakuta usafiri unahitaji ndege ambayo tiketi yake ni bei kubwa kuliko kile unacholipwa kwenye hizo shoo lakini pia ni ngumu sana kutafuta prodyuza anayeujua muziki wa Afrika. 

Swaggaz: Kwanini umekuwa ukijiita wewe ni msanii mwenye ushawishi kwenye kizazi hiki? 

Raiymek:Najiita hivyo kwa sababu ya kipaji changu kina uwezo pia nina ongoza wasanii, mimi ni baba wa muziki, nimefundisha na kuzaa Royalty Collection Company na kuwaweka kwenye ‘game’. 

Swaggaz: Marekani imeathirika sana na corona, je kwako binafsi hali ipoje? 

Raiymek: Corona imenikosesha vingi sana, kuna tamasha nilitakiwa nishiriki ila zote zimesitishwa pia radio haziwezi kutupokea wasanii kwasababu ya kukaa mbali yaani ‘kukeep social distances’. 

Swaggaz: Huwa unafananishwa na Abdukiba,unadhani kwanini na huwa unafurahia? 

Raiymek: Abdukiba ni msanii, watu wanasema tumefanana sana, hata mimi mwenyewe nimeona kweli tunafanana, watu wengi huwa wananitumia link za video za Abdukiba na kusema zamani nilikuwa na mwili mkubwa hivyo nianze kufanya mazoezi ya kunyanyua chuma na ninapo waambia sio mimi wanashangaa. 

Swaggaz: Bila shaka unafuatilia Bongo Fleva, je unatamani kufanya kazi na wasanii gani Tanzania? 

Raiymek:Natamani sana kufanya kazi na wasani wa WCB kama Diamond, Rayvanny, Mbosso pia Abdukiba na wengine wengi. 

 Swaggaz: Unawaambia nini mashabiki zako wa Afrika? 

Raiymek: Hivi karibuni nilitoa video ya wimbo wangu, Washa ambayo inafanya vizuri sana pia nina albamu yenye nyimbo nane ambapo nitaanza kuachia video moja moja kwahiyo cha kufanya mashabiki wawe tayari kupokea ngoma kali kama vile Buka Loketo, Baila Lentamente, Heri na Tuachane. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles