24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaomba kuandaa Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amesema Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji Kombe la Dunia kwa soka la watu wenye ulemavu (WAF) baada ya kumalizika inayofanyika Oktoba, 2022 nchini Uturuki.

Tanzania ni moja ya nchi iliyofunvu kushiriki Kombe la Dunia, 2022 kupitia timu ya wenye Ulemavu, Tembo Warriors ambayo imefuzu tayari baada ya kufanya vizuri  katika mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (Canaf) yanayoendelea, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Desemba 3,2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika kwa Watu Wenye Ulemavu (FAAF), jijini ambao pamoja na mambo mengine una lengo la kuwachagua viongozi wakuu wa shirikisho hilo, Bashungwa ameomba kufikiriwa kwa Tanzania kuandaa Kombe la Dunia.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania watu wenye ulemavu, wakishangilia siku walipofunvu Kombe la Dunia baada ya kuichapa Cameroon mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Da es Salaam.

Amesema Tanzania ina mazingira  wezeshi  ya kuweza kuendesha mashindano makubwa.

Aidha amewataka  washiriki wa mkutano huo kutumia mashindano hayo kuelimisha dunia kupinga ubaguzi na mila potofu za kuwatenga na kuwabagua watu wenye ulemavu kwa kuwa ni binadamu sawa na wengine na kwamba wanauwezo sawa.

Pia ametumia mkutano huo kukaribisha mataifa ya Afrika kuja kutembelea Mlima Kilimanjaro na vivutio mbalimbali vya utalii ikiwa ni pamoja na utalii wa baharini katika kisiwa cha Zanzibar.

Naye Makamu wa pili wa Shirikisho la Soka Duniani kwa Wenye Ulemavu (WAF), Mateus Wildack ametuma salamu za pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mahiri wa kuiletea Tanzania maendeleo ya haraka na kuwashirikisha kikamilifu na wenye ulemavu na kuwapa kipaumbele kwenye maendeleo hayo ikiwa ni pamoja na eneo la michezo ambayo imefanya vizuri sana.


Wasanii wa kikundi cha  Safi  wakitoa burudani  kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika kwa Watu Wenye Ulemavu (FAAF), leo Desemba 3, 2021 Jijini Dar es Salaam.
 

Ameisifia Serikali kwa uratibu makini iliyofanya kwenye mashindano ya Afrika na kueleza kuwa yamefanyika kitaalamu.

Rais wa Shirikisho hilo wa Afrika (FAAF) Mchungaji Richard Nii Adesah, amepongeza Serikali ya Tanzania kwa  ushirikiano na uwezeshaji iliyotoa katika kipindi chote cha mashindano ambapo amesema mkutano huo utasaidia kuleta mabadiliko makubwa  kwenye michezo ya walemavu katika Bara la Afrika.

Aidha ameyataka Mataifa yote ya Afrika kutokubali kugawanywa na kitu chochote kutokana na umoja imara uliojengeka baina ya nchi zote kupitia mashindano hayo ya Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles