21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaadhimisha Siku ya Kupinga Unyanyapaa na Ubaguzi Duniani

Na Nadhifa Omary, Dodoma

Tanzania imeungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha Siku ya Kupinga Unyanyapaa na Ubaguzi Duniani yanayoadhmishwa kimataifa Machi Mosi ya kila mwaka ili kuendelea kuangazia na kupaza sauti juu ya kupinga vitendo vya unyanyapaa.

Sehemu ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka yaliyofanyika Machi 1,2023 jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 1,2023 jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene.

Kupitia hotuba yake Simbachawene amesema kuwa ubaguzi na kukosekana Usawa na Haki ni miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii yanayosababisha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.

Mhe Simbachawene amesema Dhana na vitendo vya Ubaguzi vinavyoashiria Ukatili na kutokuwepo kwa usawa vinasababisha kutotimia kwa malengo yetu ya kitaifa ya mwitikio wa VVU na UKIMWI na kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kutokomeza UKIMWI.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni “TOKOMEZA UBAGUZI, OKOA MAISHA ambapo inatutaka kuangalia umuhimu wa kuhakikisha tunatokomeza ubaguzi na unyanyapaa miongoni mwa watu wanaoishi na VVU na makundi mengine.

Aidha ameeleza  kuwa kukosekana kwa usawa, uwepo wa mila zilizopitwa na wakati, ubaguzi, kutengwa na unyanyapaa kwa namna mbalimbali vyote hivi vinachangia kasi ya maambukizi mapya ya VVU.

Ameeleza kuwa Takwimu zinaonyesha usawa wa kijinsia, mila hatarishi na ukatili ni wanawake na wasichana ndio wahanga wakubwa.

Mwakilishi wa UNAIDS, Dk. Grace Mallya,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka  yaliyofanyika Machi 1,2023 jijini Dodoma.

“Baadhi ya wanawake na wasichana wamepata maambukizi ya VVU kutokana na ukatili wa kingono, Wanawake wenye VVU wapo katika hatari ya ukatili hasa baada ya kuweka wazi hali zao za maambukizi,” amesema Simbachawene.

Kadhalika, amesema tabia, mila na desturi  hatarishi vimepelekea kukosekana kwa usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia Tanzania, hali hiyo inachochea na kuongeza kiwango cha maambukizi na baadhi ya matukio yanayosababisha kuambukizwa na kusambaza VVU, kati ya wanawake na wasichana.

Vile vile, amesema  wanawake wameathirika zaidi kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usawa katika uhusiano wa kijinsia na majukumu ya kijinsia pamoja na kutopewa fursa ya kufanya maamuzi.

“Ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uwezo wa kujadili juu ya matumizi ya kondomu na ngono salama, vipengele hivi husababisha ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili wa kijinsia,”amesema.

Hata hivyo, amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la NACOPHA wameweza kufanikisha kuhamasisha watu wanaoishi na VVU kujiunga kwenye konga ambapo hushirikiana pamoja kujikwamua kiuchumi, kupeana taarifa mbalimbali, na hata kuhudumiana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, akizungumza Machi 1,2023 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka.

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wadau wote na mashirika yanayotoa msaada kwa watu wanaoishi na VVU na watoto yatima. Aidha nawapongeza TACAIDS na Baraza la watu wanaoishi na VVU kwa kuendelea kusimamia maslahi pamoja na haki za ustawi wa watu wanaoishi na VVU nchini,” amepongeza Simbachawene. 

Pia amesema Serikali imehakikisha Dawa za ARV zinaendelea kupatikana nchini bila kikwazo chochote, hivyo wale wote wanaogundulika kuwa na VVU waanze na waendelee kutumia ARV kama inavyooelekezwa na wataalamu wa Afya.

“Natoa rai kwa watoa huduma wote kuepuka vitendo vya kunyanyapaa na lugha za kudhalilisha WAVIU pindi wanapohitaji kuhudumiwa. Suala hili la unyanyapaa na ubaguzi linarudisha nyuma jitihada za kuutokomeza UKIMWI”, amesisitiza Simbachawene

Simbachaene amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeweka sera na mifumo mizuri ya kisheria, mipango ya kitaasisi na miongozo ya kitaifa ambayo imetengeneza mazingira mazuri ya kuboresha haki za binadamu, usawa wa kijinsia pamoja na ushirikiano wa jamii.

Kupitia Wizara ya Jinsia Wanawake na watoto mwaka 2000 serikali ilitunga Sera ya Maendeleo ya Wanawake na jinsia na mpango mkakati wa kijinsia ili kuhamasisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa jamii.

Sera hiyo pia inaongelea kuhusu unyanyasaji wa wanawake na watoto kupitia mkakati wake wa kijamii kwa ajili ya kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya maambukizi ya VVU.

Naomba kutoa wito kwa TACAIDS na wadau wake kuangalia jinsi gani mnaweza kuandaa jumbe kwa makundi yote ikiwemo matumizi ya maandishi ya nukta nundu kutoa elimu kwa kundi hili.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa NACOPHA, Yusuph Marere, amesema Katika maadhimisho hayo wanaungana na wenzao duniani kote kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa kuzingatia heshima na utu wa binadamu pasipo kuwa na ubaguzi wa aina yoyote.

“Siku hii muhimu inatukumbusha kuwa kila mmoja anapaswa kuheshimu na kuheshimiwa na vilevile inatukumbusha kuwa na mifumo, sera na huduma jumuishi zinazohusisha makundi yote katika jamii na pia tunakumbushwa kupinga aina zote za unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU na watu walio katika makundi maalumu,” amesema Marere.

Ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa unyanyapaa na ubaguzi katika jamii umechangia watu wengi kushindwa kujitokeza ili kupata huduma bora za VVU na UKIMWI ikiwemo upimaji wa hiari wa VVU,tiba na matunzo.

Amesema Juhudi za dhati zinahitajika ili kukomesha hali hii katika taifa letu na kwa kufanya hivyo tunaweza kufikia malengo ya dunia ya kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.

Naye mwakilishi wa UNAIDS Dk. Grace Mallya amesema kuwa mwaka 2021 makakati wa kidunia wa UKIMWI na tamko wa kisiasa a UN ililiridhia na kuanisha mikakaati mbalimbali ikiwemo kuondoa ubaguzi unaochochewa na sera na sheria mbambali mpaka chini ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

“Unynyapaa huchangia hatari ya kuongeza maambukizi ya UKIMWI, kuongeza au kupunguza ufanisi wa dawa za VVU na kuongeza vifo vinavyotokana na UKIMWI, hali inayorudisha nyuma hatua ambazo nchi imeishazipiga katika kuumaliza UKIMWI ifikapo  2030,” alisema Dk. Mallya

Tafiti zinaonesha nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania, kiwango kikubwa cha Maambukizi hasa kwa vijana wa miaka 10 hadi 24 na makundi maalum. Aidha kiwango kikubwa cha watoto chini ya miaka miwili wanaoishi na VVU hawapo  kwenye dawa hivyo basi ni muhimu kuondoa ubaguzi unaoweza kurudisha nyuma hatua zilikwishapigwa .

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Jumanne Issango akimkaribisha Mgeni rasmi alisema TACAIDS kwa kushirikiana na wadau wameandaa maadhmisho hawa ikiwa ni hatua ya kendelea kukumbushana na kuondoa vitu vinavyochangia unyanyapaa na ubaguzi na kuchochea ongezeko la maambukizi ya VVU.

Issango amesema kuwa kupitia maamzimisho haya kuna mambo tutajifunza na kuondokanayo ili kwa lengo la kuendelea kuelimsha jamii juu ya athari za unyanyapaa na ubaguzi katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles