25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Uholanzi zasaini kuinua sekta mifugo, uvuvi

MWANDISHI WETU-ARUSHA

SERIKALI ya Tanzania na Uholanzi zimesaini makubaliano  ya miaka mitano ya kusaidia kuinua maendeleo na ukuaji wa sekta za mifugo na uvuvi nchini.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa jana jijini Arusha yana lengo la kuona sekta za ufugaji kuku na samaki zinapata mwamko stahiki kwenye mifugo na uvuvi kwa kuwajengea uwezo Watanzania wa kujikita katika uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo,  Naibu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Marjolijn Sonnema, alisema mpango huo utafanikishwa kupitia maofisa ugani nchi nzima.

“Wafugaji watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kunufaika na mradi huu ambao utaongeza uzalishaji wa chakula na biashara.

“Wataalamu watawafundisha wakulima namna bora ya kuboresha ufugaji wa kuku na ufugaji wa kisasa wa samaki katika sekta hizi mbili za mifugo na uvuvi,” alisema Sonnem.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alisema mkataba huo una maana kubwa kwa Tanzania kama nchi kwani utaongeza uzalishaji na kuinua maisha ya mfugaji.

“Makubaliano haya yanalenga kuhamasisha ulaji wa samaki na kuku ambao upo chini sana miongoni mwa Watanzania wengi,” alisema Ulega.

Alisema Tanzania inavuna kiasi cha tani 350,000 za samaki kwa mwaka ukilinganisha na mahitaji halisi ya tani 700,000.

“Kwa takwimu hizi zinaonesha kuwa ni kiasi kidogo sana cha virutubisho tunachotoa kwa kutokana na kuku na samaki,” alisema.

Ulega alisema kuwa bado kuna dhana potofu miongoni mwa Watanzania wengi kuwa ulaji wa samaki bado ni kitu cha anasa na si kwa ajili ya virutubisho mwilini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles