28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Pakistan zasaini mikataba ya makubaliano ya kidiplomasia

Na MwandishiWetu, Dar es Salaam

Tanzania na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba wa mashaurino ya kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiuchumi.

Mikataba hiyo imesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa fursa nyingi zilizopo za kuongeza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Pakistan hasa katika sekta ya kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite, pamoja na uwekezaji.

“Tanzania na Pakistan zina uhusiano wa muda mrefu na katika mazungumzo yetu ya leo, Balozi wa Pakistan ameeleza fursa zilizopo Pakistan ambapo fursa hizo zikitumiwa vizuri zitanufaisha mataifa yote mawili,” amesema Prof. Kabudi 

Prof. Kabudi ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Pakistan na kwamba fursa hizo zitaendelea kuongeze ushirikiano wa diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

Kwa Upande wake Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mohammad Saleem amesema kuwa kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu itasaidia kukuza na kuendeleza diplomasia ya Uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.

“Ni imani yangu kuwa kusainiwa kwa mikataba hii miwili ya makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Pakistan kutasaidia kudumisha na kukuza uchumi kati ya mataifa yetu,” amesema Balozi Saleem

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles