31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania Kwanza yazidi kumwandama Balozi wa Ujerumani

Mwenyekiti wa Kamati ya Tanzania Kwanza ya Nje ya Bunge la Katiba, Agustino Matefu
Mwenyekiti wa Kamati ya Tanzania Kwanza ya Nje ya Bunge la Katiba, Agustino Matefu

NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

KUNDI la Tanzania Kwanza nje ya Bunge Maalumu la Katiba, limemtaka Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, kuacha kutoa majibu mepesi kwa maswali mazito yanayoihusu Tanzania.

Aidha, limemtahadharisha Balozi Kochanke kama asipozionya taasisi za nchi yake zinazotuhumiwa kutoa fedha za kuvuruga Katiba mpya, wataandamana hadi nje ya ubalozi huo kushinikiza afukuzwe nchini.

Ofisa Mawasiliano wa Ubalozi wa Ujerumani, John Merikion, alitoa ufafanuzi wa madai ya Mwenyekiti wa Kundi la Tanzania Kwanza, Agustino Matefu aliyeituhumu

nchi hiyo kuwapa fedha wanasiasa na vyama vya siasa ili wavuruge Katiba mpya.

Katika ufafanuzi wake, Merikion alisema Serikali ya Ujerumani kimaadili haiingilii mambo ya siasa za ndani za nchi nyingine.

Hata hivyo, majibu hayo yameelezwa na Matefu kuwa ni mepesi kulingana na  maswali magumu waliyomuuliza Balozi Kochanke.

Kutokana na kutolewa kwa majibu hayo, Matefu alikutana na waandishi wa habari jana jijini hapa na kumtaka balozi huyo kuziita na kuzionya taasisi zinazotoka nchini kwake ambazo zinadaiwa kutoa fedha hizo.

“Vyama vinavyounda Tanzania Kwanza CCM, CCK, TLP, Chauma, Chausta, Jahazi Asilia, FAO, UDP, APPT Maendeleo vimenituma kumwambia Balozi Kochanke asipozishauri hizo taasisi zake tutafanya maandamano kushinikiza afukuzwe nchini kwetu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles