Na Mwandishi wetu   |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga amesema Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limekubali kununua mahindi yanayolimwa nchini na kuyapeleka katika nchi za Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), na Somalia ambako kuna njaa.
Kutokana na hali hiyo amesema wakulima hawana haja ya kuhofia soko la mahindi yao kwa kuwa serikali imesharuhusu wakulima kuuza mahindi yao nje ya nchi na kwa wanunuzi wanaowataka.
Naye waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba akizungumzia eneo hilo amesema WFP wameingia mkataba na Wakala wa Taifa wa Ghala la Taifa (NFRA), kwa ajili ya kununua tani 31,000 za mahindi yatakayopelekwa katika nchi hizo.
Mahiga na Dk. Tizeba wameyasema hayo leo Mei 16, bungeni jijini Dodoma, walipokuwa wakijibu hoja ya Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema), aliyekuwa ameonyesha nia ya kukwamisha bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Ununuzi wa mahindi uharikishwe kwa kuwa hata mahindi ya mwaka jana bado yapo mitahani