24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania, Kenya zazindua mpango kudhibiti homa ya bonde la ufa

Janeth Mushi, Namanga

Tanzania  na Kenya zimezindua zoezi la jaribio la pamoja la kudhibiti magonjwa ya milipuko (homa ya bonde la ufa) katika maeneo ya mipakani ikiwemo magonjwa yanayoenezwa na binadamu, mifugo na wanyama kama Ebola.

Uzinduzi huo ulifanyika jana Juni 11, katika mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga, zoezi lililoratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani(GIZ).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo litakalofanyika kwa siku nne, Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu, alisema  hatua hiyo inalenga kupima uwezo wa kukabili magonjwa hayo kama yatatokea huku wananchi wakitajwa kuwa wadau wakubwa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa haraka pindi magonjwa hayo yanapotokea katika maeneo yao.

Alisema kupitia zoezi hilo wanachoangalia ni kujitathmini kama vifaa vinatosha, kuwepo kwa wataalamu watakaoweza kuhudumia wagonjwa pindi magonjwa yanapotokea.

Awali Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alisema Wizara yake imejipanga vizuri dhidi ya magonjwa ya milipuko kwa wanyama ambapo kwa sasa wamefanikiwa kudhibiti ugonjwa wa kimeta unaoathiri mifugo kwa kuwa na chanjo ya ugonjwa huo inayotoka taasisi ya TVI, Kibaha.

Alisema kutokana na biashara ya mifugo kufanyika katika nchi jirani ya Kenya, aliwataka wananchi kuondoa hofu juu ya mifugo hiyo kwani kabla haijapelekwa inafanyiwa ukaguzi na vipimo mbalimbali.

” Kuna wataalamu wa kutosha wanaoshughulikia magonjwa haya pindi yanapotokea ambapo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo cha maafa, na mifugo yetu ni salama kwani wataalamu wetu kila mara wanashirikiana na wafugaji wetu na mifugo hukaguliwa mara kwa mara na kama kuna matatizo imekuwa ikishughulikiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles