25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA IWEKE AJENDA YA KUONGEZEKA FAIDA ZA DIASPORA

Na, SARAH MOSSI


MAPEMA mwaka jana nilibahatika kutembelea nchi ya Sweden kwa mwaliko wa  Watanzania waishio katika nchi hiyo. Moja ya ajenda kubwa ya safari yangu ni kwenda kuangalia shughuli mbalimbali za kimaendeleo wanazozifanya Watanzania wenzetu ‘Diaspora’katika nchi hiyo.

Nilibahatika kumtembelea mmoja wa Watanzania mwenye ujuzi wa hali ya juu na anayeaminiwa na Serikali ya Sweden, Dk. Mselly Nzotta Mbwambo (PhD)ambaye ni mtaalamu wa mchakato wa madini katika kiwanda maarufu cha Uddeholm katika mji wa Kalstard

Mchango wa wanadiaspora kwa maendeleo ya nchi unazidi utoaji wa  fedha na diaspora kwa mtu binafsi katika nchi yake. Hii ni kweli kwa sababu wanadiaspora wanaweza kuwa chanzo muhimu na kutoa usaidizi wa utafiti na uvumbuzi, uhamisho wa teknolojia  na maendeleo ya ujuzi. Japan, Jamhuri ya Korea na Taiwan, China ni mifano ya uchumi ambayo  ulitegemea wanadiaspora wao kama vyanzo vya ujuzi.  Serikali katika  nchi hizi, ili kuinua uchumi wao,nchi zilihimiza kurudi kwa wanafunzi wenye  elimu ya kigeni au hata kuanzisha mitandao ya kubadilishana maarifa  kati ya Serikali na wanadiaspora.

Katika jaribio la kuelewa uwekezaji, viungo vya biashara, ujuzi na uhamisho wa teknolojia – ambayo wanadiaspora kama rasilimali za nchi yetu (zaidi ya utoaji wa fedha) wanaweza kuhamasishwa kwa maendeleo ya Tanzania nilipotembelea Sweden kikazi kuzungumza/kuwahoji diaspora, wenye ujuzi na wenye ujuzi wa juu kwani wote wanatoa michango kwa nchi yao.  Kwa sababu Serikali imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kufikia lengo la dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025, nilibahatika kuhojiana na Mtanzania Dk. Mselly Nzotta Mbwambo (PhD)ambaye ni mtaalamu wa mchakato wa madini (Process Metallurgy) (pichani akifanya research). Dr. Mselly Nzotta Mbwambo alinieleza umuhimu wa Metali katika maisha yetu.

 

“Ikiwa unapenda au la, metali zinacheza sehemu  kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Tunashirikiana nazo tofauti kwa kuwa kila moja ina umuhimu wake wa pekee: baadhi hutumiwa kusaidia kwenye majengo, simu za mkononi (Smarthones), usafiri. Baadhi hutumiwa kwa ajili ya mapambo au baadhi hutumiwa kuonesha utajiri, kama vile dhahabu kwa mfano,”

Dk. Mselly alisema, “Tanzania inatakiwa kujitegemea katika ujuzi wa mchakato wa madini ili  Mtanzania Dk. Mselly Mbwambo Nzota ambaye ni mtaalamu katika mambo ya utengenezaji  chuma Mtanzania Dk. Mselly Mbwambo Nzota ambaye ni mtaalamu katika mambo ya utengenezaji  chumamahojiano kati ya Mwandishi SARAH MOSSI aliyefanya ziara ya kikazi nchini Sweden hivi karibuni na Mtanzania Dk. Mselly Mbwambo Nzota ambaye ni mtaalamu katika mambo ya utengenezaji  chumakuwa na ujuzi wa kupambana  na watendaji wa kimataifa na kuepuka makosa ya muda mfupi na pia kugundua teknolojia za kuchimba madini yetu.  Kwa mfano Serikali inatambua kwamba mradi wa chuma Liganga kuwa nyenzo na msingi mkuu wa uchumi wa viwanda nchini. Mfano, madini ya chuma ya Liganga ni ya pekee na ilitakiwa/inatakiwa sisi kama Watanzania tuwe na ujuzi wetu wa kuchuja Fe,  ferro-titanium  (Fe-Ti) na ferro-vanadium (Fe-V) bila kupoteza  kwenye makapi metali zenye thamani kama Titanium (Ti) na Vanadium (V)”. Madini ya Chuma ya Liganga (iron ore) ni Fe-V-Ti system. Bei ya chuma ukilinganisha na Vanadiunm (V) na Titanium (Ti) ni masikitiko. Bei ya Iron Ore fines ni 69,00 USD/t (0,069 USD/kg), ferro-titanium ni 3770 USD/t (3,77 USD/kg) and ferro-vanadium ni 22600/t(22,6 USD/kg). Source: hpp:www.infomine.com/investment/metal-prices/ferro-vanadium/” 

Steel Raw Material Prices
Cobalt USD/Ib 29.26
Ferro-Chrome USD/kg 2.48
Ferro-Titanium USD/kg 3.77
Ferro-Tungsten USD/kg 25.52
Ferro-Vanadium USD/kg 22.60
Iron Ore Fines USD/t 69.00
Iron Ore Pellets USD/t 96.06
Nickel USD/Ib 5.26
Tin USD/Ib 8.66

“Kwa nini mtazamo wa Serikali usiwe namna ya kupata ferro-vanadium au ferro-titanium,” alihoji Dk. Mselly. “Au ferro-vanadium au ferro-titanium zitakwenda kwenye makapi ya chuma (matatizo ya mazingira na ya uchumi); au itakuwa kama suala la mchanga wa dhahabu,”   “Kuna viongozi nilizungumza nao kuhusu suala la Vanadium (V) na Titanium (Ti) ila sijasikilizwa” alisema Dk. Mselly. Sera ya kutumia wataalamu wetu hasa diaspora inatakiwa iangaliwe kwa makini. Bado sera hii ina utata. Wawekezaji wa kigeni hupewa kipaumbele kuliko kwa wanadiaspora. Ingekuwa vizuri zaidi kuwa na taratibu za kuangalia ufanisi kwa wawekezaji wote, bila kujali asili ya mwekezaji na utaifa.  Mwisho…..     mahojiano kati ya Mwandishi SARAH MOSSI aliyefanya ziara ya kikazi nchini Sweden hivi karibuni na Mtanzania Dk. Mselly Mbwambo Nzota ambaye ni mtaalamu katika mambo ya utengenezaji  chuma

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles