32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA HATARINI KUPOTEZA SOKO LA MADINI YA VITO

Na Masyaga Matinyi – Arusha


TANZANIA ipo katika hatari ya kupoteza soko la madini ya vito baada ya Kenya kufuta ushuru wote pindi yanapoingia nchini humo.

Hatua hiyo ya Kenya imefikiwa katika mkutano maalumu kuhusu sekta ya madini (Kenya Mining Forum) uliofanyika jijini Nairobi, Desemba 4 hadi 5, mwaka huu na kuhudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na Waziri wa Madini, Dan Kazungu.

Katika mpango mkakati uliotangazwa katika mkutano huo ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 200 kutoka mataifa mbalimbali, Serikali ya Kenya ilisema inafungua mipaka yake ili kuruhusu madini ya vito kuingia bila vikwazo vyovyote.

“Kufungua mipaka ya Kenya kuruhusu madini ya vito kutoka ukanda wa Afrika kuingia Kenya kwa uhuru bila vikwazo,” ilisema sehemu ya mpango mkakati.

Pia katika mkutano huo, Serikali ya Kenya ilisema inaunda Shirika la Madini la Taifa huku ikikusudia kulifanya kuwa shirika kubwa la madini barani Afrika.

Mbali na kulifanya kuwa shirika kubwa Afrika, pia itahakikisha linasajiliwa katika masoko makubwa ya hisa duniani, ambayo ni New York Stock Exchange (NSE) na London Stock Exchange (LSE), lengo likiwa kupata mitaji ya uwekezaji katika sekta ya madini.

Wakati Kenya ikipanga mikakati hiyo yenye lengo la kuifanya kitovu cha biashara ya madini ya vito katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania imekuwa ikitoza ushuru kwa madini kama hayo yanayoingizwa nchini wakati wa maonyesho yanayofanyika jijini Arusha.

Madini ya vito yanayoingizwa nchini hutozwa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini (import duty) kutokana na ukubwa wa mzigo.

Alipoulizwa kuhusu hatua ambazo Tanzania inachukua au itachukua kukabiliana na changamoto hiyo, Waziri wa Madini, Angela Kairuki, alisema wizara yake ilipeleka mwakilishi katika mkutano huo Nairobi na ripoti inafanyiwa kazi.

“Siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja sasa, tulituma mwakilishi, hivyo tunasubiri ripoti yake, kisha tutakaa na kuangalia nini cha kufanya kwa masilahi ya taifa,” alisema Kairuki.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere, alisema ameipokea taarifa hiyo na watakutana na wadau wengine serikalini ili kutafuta mwafaka wa kukabiliana na changamoto hiyo ya kibiashara na uchumi.

Kwa habari kamili nunua nakala yako ya MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles