29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MUKOBA WA CWT ADAKWA KWA RUSHWA

Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

NA MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inamshikilia Rais mstaafu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, kwa tuhuma za kutaka kuwahonga wapigakura katika uchaguzi wa chama hicho unaofanyika Ukumbi wa Chimwaga, Dodoma.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba, alisema Mukoba alikamatwa jana saa tatu asubuhi akiwa katika mchakato wa kuwashawishi wajumbe kumpigia kura mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais, ambaye jina lake hakuweza kulitaja kutokana na sababu za kiuchunguzi.

“Alionekana ukumbini akiwashawishi wajumbe wampigie kura mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais na baadae watawapa kitu kidogo,” alisema.

Misalaba alipoulizwa kama walimkuta na kidhibiti chochote, alisema kuwa taratibu zinawaruhusu kumkamata mtu   anayeonyesha viashiria kabla ya hajasababisha madhara katika eneo husika.

Uchaguzi huo unafanyika wakati chama hicho kikiwa na viongozi wanaokaimu.

Nafasi ya urais anakaimu Leah Ulaya baada ya chama hicho kutoa tangazo la kusitisha ajira za Mukoba na Naibu Katibu Mkuu wake, Ezekiel Olouch.

Juzi, Rais Dk. John Magufuli alifungua mkutano wa chama hicho na pamoja na mambo mengine, alitishia kuifuta ama kuifilisi Benki ya Walimu baada ya mwelekeo wake kutoridhisha.

Magufuli alisema benki hiyo ipo katika orodha ya benki zenye mwelekeo wa kufutwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles