24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TanTrade wakutana na wadau wa ngozi nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kushiriki kikao cha wadau wa ngozi hapa nchini kilichowajumuisha wataalam kutoka Taasisi ya Ushirikiano ya Kijerumani (GiZ leather technical team).

Kikao hicho kilifanyika Aprili 26, 2022 kwa lengo la kujadili hatua za awali za utekelezaji wa Mradi wa ‘Support towards Industrialization and Productive Sectors’ ambapo sekta ya ngozi ni miongoni mwa zilizopewa kipaumbele.

Mradi huo utatekelezwa katika nchi wanachama wa SADC kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

TanTrade iliwakilishwa na wataalam kadhaa wa sekta ya ngozi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Emmanuel Miselya, ambaye aliwaeleza wadau wa ngozi kuwa mamlaka hiyo ipo tayari kushirikiana nao kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuleta tija kuanzia mfugaji hadi muuzaji wa bidhaa za ngozi.

Kwa upande wake mtaalam kutoka GiZ, Klaus Heinze, amesema sekta ya ngozi bado ina fursa kubwa kwa soko la ndani ya nchi na katika soko la SADC kwani bidhaa nyingi za ngozi zinaingizwa katika soko hilo kutoka mataifa ya mbali.

“Namna bora ya kuhakikisha sekta hii inakua ni kuhakikisha mnyororo wa thamani unasimamiwa ipasavyo kwa kila hatua,” amesema Heinze.

Naye Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi nchini, Freddy Kabala, alitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa ngozi zenye ubora, utaalam duni wa uzalishaji pamoja na mitaji.

Amesema changamoto hizo zinasababisha bidhaa zinazozalishwa nchini kuonekana kuwa ghali na hivyo kupunguza uzalishaji na kutoa mwanya kwa bidhaa nyingi kutoka nje ili kuziba pengo kubwa lililopo.

Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe zaidi ya nilioni 33.4 na mifugo mingine kama mbuzi na kondoo zaidi ya milioni 30 wakati uzalishaji wa viatu vya ngozi ni wastani wa jozi milioni tatu huku jozi milioni 54.3 za viatu vya ngozi vikiingizwa nchini kutoka mataifa mengine ya Ulaya na Asia kwa mwaka.

Mpaka Sasa kuna viwanda vinne vikubwa vinavyozalisha bidhaa za ngozi nchini ambavyo ni Bora Industries, Woiso Original Products (WOP), Ital Shoes na Kilimanjaro Leather International Company Industries Ltd.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles