29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TANROAD simamieni kwa karibu miundombinu ya barabara-Kasekenya

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mbunge wa Ileje na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amewaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROAD) Mkoa wa Songwe kuhakikisha wanasimamia kwa karibu miundombinu ya barabra.

Aidha, amewataka kutatua changamoto ya kuziba kwa kalavati katika barabara ya Isongole- Kasumulu na Ibungu -Tukuyu ili kuondoa adha kwa watumiaji.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ileje, Ubatizo Songa.

Mhandisi Kasekenya amesema hayo Machi 4, 2022 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake, ikiwepo barabara zinazosimamiwa na TANROAD na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) wilayani humo.

Amesema wananchi wa Tarafa ya Bundali hukumbwa na changamoto ya kutumia barabara hizo kutokana na magari kukwama hususan kipindi hiki cha masika kutokana na makalavati kujaa maji baada ya kuzibwa na tope, hivyo kuagiza kutatua shida hiyo kwa wakati.

“Naagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe kufanya ukaguzi wa makalavati yote yaliyozibwa na kuyazibua ili wananchi waendelee kutumia barabara hizo ambazo zimekuwa chachu ya kuwaongezea kipato wananchi kutoka Ileje na wilaya za jirani Kyela na Rungwe,

“Pia imekuwa na msaada kwa wananchi wa Malawi kupitia boda ya Isongole Ileje na boda ya Kasumulu hadi kyela mkoani Mbeya,” amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha, waziri Msongwe amesema ya Rais Samia Suluhu Hassan, ipo katika hatua ya upembuzi na usanifu kwa ajili ya kulima barabara kwa kiwango cha lami kutoka Isongole hadi Ileje mkoa wa Songwe mpaka Kasumulu hadi Kyela mkoa wa Mbeya yenye urefu wa zaidi ya  kilomita 90 ili kufungua boda hizo kibiashara na kurahisisha uzalishaji wa makaa ya mawe katika Mgodi wa Kabulo uliopo wilayani Ileje.

Baadhi ya wananchi.

Akizungumzia kero za barabara hizo diwani wa kata ya Kalembo, Leward Songa  amemuomba Naibu waziri na mbunge huyo kuzungumza na TANROAD kutenga mafungu ya kusafisha na kulima barabara kwa mapana ili magari yaweze kupishana na kuepusha ajali zinazosababishwa na uchakavu wa miundombinu kutokana na majani ya miti kutanda barabara.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ileje, Ubatizo Songa amesema licha ya TANROAD kulima barabara kwa kiwango cha changamoto iliyopo sasa ni kuziba kwa makalavati ambayo huziba kipindi cha masika hali ambayo husababisha baadhi ya sehemu kutopitika na kuleta adha kwa watumiaji wa barabara nyingi zinazosimamiwa na wakala huo wilaya ya Ileje.

“Zaidi ya makalavati kutoka Katengele mpaka Kalembo kuna zaidi ya makalavati 12 ambayo yameziba hivyo kunahitaji boksi kalavati ili kuepusha adha kwa watumiaji wa tarafa ya Bundali,” amesema Songa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles