27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kadinda ‘awang’ata sikio’ wanawamke wajasiriamali Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MBUNIFU nguli wa mavazi nchini, Martine Kadinda amewataka wanawake wajasiriamali na vijana wa wilaya ya Magharibi ‘A’, kisiwani Zanzibar, kutumia utofauti alio nao binafsi kuboresha biashara yake.

Kadinda ni miongoni mwa wabunifu wajasiriamali waliofanikiwa na kutambulisha taifa katika sekta ya mavazi na kujitwalia tuzo sita za kimataifa.

Akizungumza na wanawake wajasiriamali katika kilele cha mafunzo ya Mwanamke Fanikisha, yaliyofanyika leo Machi 5, wilayani humo, Kadinda amesema kila mtu ameumbwa na utofauti wake ni vizuri kutumia utofauti huo kutofautisha biashara yake.

“Binadamu wote ni sawa ila kila mmoja ameumbwa na utofauti wake, tunaweza kufanya biashara moja ila ukaitofautisha na nyingine kulingana na utofauti ulio nao binafsi ikavutia wateja wengi kwa sababu kila mtu ana kitu kinachomvutia na kukipenda,” amesema Kadinda.

Ameongeza kwa kutoa mfano kwamba wote wanaweza kukaanga mihogo mmoja akaweka chachandu ya mbilimbi mwengine akaweka ya embe hapo tayari kunakuwa kunatofauti nakwamba biashara zao kila mmoja atakuwa na wateja wake.

Aidha amesema Zanzibar ni kisiwa ambacho kina fursa nyingi za biashara hasa kwa wanawake kwa sababu kuna watalii wengi tofauti na Tanzania Bara.

“Tunapaswa kutumia fursa ya wageni kutoka nchi tofauti kujikwamua kwa kubuni biashara ambazo zitawavuta zaidi watalii, niombe serekali kuandaa tamasha kama hili ambalo litawaleta wakufunzi wengi kuja kutoa elimu kwa wanawake wa Zanzibar,” amesema Kandinda.

Semina ya Mwanamke Fanikisha, imefanyika kwa wiki moja ili andaliwa na mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, kwa wanawake na vijana ili kuboresha biashara zao na kujikwamua katika wimbi la umasikini na utegemezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles