23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO kutumia 12 bilioni ujenzi kituo cha umeme Ushetu

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatarajia kutumia kiasi fedha sh. 12 bilioni kwa ajili ya kujenga kituo kidogo cha umeme (Switching Station) kwenye Wilaya ya Ushetu eneo la Nyamirangano ili kuboresha hali ya upatikanaji wa nishati hiyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, . Dk. Doto Biteko wakati akijibu swali la Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani aliyeuliza, Je nini mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme wa uhakika katika Halmashauri za Ushetu, Msalala, na Kahama?

Judith amesema pamoja na kituo hicho, TANESCO itaongeza njia nyingine za umeme kutokea kituoni hapo kwenda Ushetu, Msalala, na Kahama ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

“Ujenzi wa mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 12 na mradi unategemewa kukamilika katika mwaka wa fedha 2024/2025, “amesema Kapinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles