24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco kushusha bei ya umeme

DSC_0828Na Jonas Mushi

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imepunguza na kufuta baadhi ya tozo mbalimbali za huduma ya umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felex Ngamlagosi, alisema mabadiliko hayo yameanza kutumika tangu jana Aprili mosi.

Aliziotaja tozo zilizofutwa kuwa ni pamoja na ile ya mwezi kwa wateja wa majumbani (T1) ya sh 5,520 na ile ya kuwasilisha maombi ya kuunganishiwa umeme ya sh 5,000.

Alisema mabadiliko hayo yametokana na mabadiliko ya bei ya mafuta, thamani ya fedha na mfumuko wa bei na kwamba yamefanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 7 ya Urekebishaji wa Bei za Umeme ya mwaka 2016 ambapo tozo hizo zimepungua kwa asilimia 1.5 hadi 2.4 ikilinganishwa na bei za sasa.

Alisema marekebisho ya bei ya umeme kwa mwaka 2017 yameahirishwa hadi Shirika la Umeme Tanesco litakapowasilisha upya maombi kabla ya Agosti 31 mwaka huu.

“Kufuatana na kifungu cha Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, kifungu cha 23(2) na 23(3), yatakuwepo marekebisho ya bei ya umeme kutokana na mabadiliko ya bei ya mafuta, thamani ya fedha na mfumuko wa bei,” alisema Ngamlagosi.

Alisema gharama za urejeshaji umeme kwa wale waliokatiwa ni sh 7000 huku tozo ya kurubuni mfumo wa mita za umeme kwa wateja wa D1, T1, T2 na T3 itakuwa kama ilivyoanishwa kwenye kanuni za huduma ya ugavi wa umeme.

Aidha alisema agizo hili linafuta agizo Na. 013_007 la Disemba 10 2013 la TANESCO pamoja na marekebisho ya agizo yaliyofuata kuhusu marekebisho ya bei za Umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles