23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tammy, Mount wavunja rekodi Chelsea

LONDON, ENGLAND

WACHEZAJI chipukizi wa timu ya Chelsea, Tammy Abraham na Mason Mount, wamevunja rekodi iliyowekwa miaka 27 iliopita ya kuwa wachezaji wenye umri mdogo nchini England chini ya miaka 21 kufunga mabao kwenye mchezo mmoja katika kikosi hicho.

Chelsea juzi ilishuka dimbani dhidi ya Norwich City katika michuano ya Ligi Kuu nchini England na kufanikiwa kushinda mabao 3-1 ambayo yaliwekwa wavuni na Abraham akifunga mawili huku lingine likifungwa na Mount.

Mara ya mwisho kwa wachezaji wa Chelsea wenye umri chini ya miaka 21 kufunga mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ilikuwa mwaka 1992.

Baada ya ushindi huo wa juzi, kocha wa Chelsea, Frank Lampard ameweka wazi kuwa, wachezaji chipukizi watakuwa na nafasi kubwa kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya usajili baada ya kufungiwa na shirikisho la mpira wa miguu la kimataifa (FIFA).

Hata hivyo aliongeza kwa kusema, Abraham na Mount watakuwa kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo mwingine mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Sheffield United.

“Hutukufanya usajili hiyo inajulikana kutokana na kufungiwa na shirikisho la soka la kimataifa, lakini wachezaji waliopo ninaamini wanaweza kufanya makubwa kwenye michezo mbalimbali inayofuata.

“Abraham na Mount watapata nafasi kubwa kwenye kikosi kutokana na jinsi wanavyojituma kwa ajili ya timu, hata hivyo bado ni wadogo wanahitaji kucheza michezo mingi ili waweze kupata uzoefu wa kutosha,” alisema Lampard.

Aliongeza kwa kusema, baada ya kuondoka Eden Hazard, timu hiyo imekuwa na wakati mgumu wa kuziba nafasi ya mchezaji huyo kwa mtu mmoja mmoja, lakini atahakikisha anawatengeneza wachezaji waliopo kucheza kwa umoja ili kuziba nafasi hiyo.

“Hazard alikuwa na mchango mkubwa ndani ya timu, kuondoka kwake kwa timu ambayo haijafanya usajili ni pengo kubwa, lakini wachezaji wanatakiwa kuishi maisha mengine mapya, ninaamini umoja utaweza kuziba nafasi hiyo, lakini kwa mchezaji mmoja mmoja itakuwa ngumu,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles