23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Tambwe apania nusu fainali shirikisho

Amissi Tambwe
Amissi Tambwe

NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Yanga, Amissi Tambwe, amesema hawawezi kukata tamaa ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kupoteza michezo miwili mfululizo katika Kundi A.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao waliingia hatua ya makundi baada ya kuiondosha Sagrada Esperanca ya Angola hatua ya 16 bora, walifungwa bao 1-0 na Mo Bejaia ya Algeria ugenini kabla ya kuchapwa bao 1-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Akizungumza na MTANZANIA jana, Tambwe alisema licha ya mechi hizo kuwa ngumu watajipanga kwa michezo iliyobaki ili wapate matokeo yatakayowafikisha hatua hiyo kwani nafasi wanayo.

“Tunaomba mashabiki waendelee kutupa sapoti, pia tunawahakikishia matokeo yatakuwa mazuri kuanzia mchezo dhidi ya Medeama ya Ghana utakaochezwa Julai 15, mwaka huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles