Na Brighter Masaki, Dar es Salaam
Shindano la kusaka Mwanamke anayepika vizuri futari maarufu kama ‘Mwanamke fundi’ linatarajiwa kufanyika Mei 4, mwaka huu Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na www.mtanzania.co.tz jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Shindano hilo, Albert Kilala amesema mashindano hayo yanalenga Wanawake ambao ni Mama lishe au Ntilie
“Shindano la Mwanamke fundi litaendeshwa zaidi na wazamini kwa kushirikiana na Chanel 10 na Magic Fm, huku washiriki wakubwa wakiwa ni wamama wa mitaa tofauti tofauti.
“Zawadi mshindi wa kwanza atapata kiasi cha Sh 100,000 na zawadi nyingine zitatolewa na wazamini,” amesema Kilala.
Kwa upande wake mshehereshaji wa shindano hilo, Salma Msangi, amesema ni wakati wa Mwanamke kuonyesha uwezi wake katika mapishi hasa ya futari katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani.
“Ni mashindano ya kwanza kufanyika kwa mwaka huu tutafanya Dar es Salaam, kwa mwaka ni tutahakikisha tunaenda mikoa mingine ili kuwafikia nao kushirikiana shindano hili” amesema Salma
Shindano hilo limeungwa mkono na Azania Group kwa kuwapa unga wangano mafuta na bidhaa mbalimbali zitakazowaidia wanawake kuweza kutengeneza vyakula mbalimbali.