23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Tamthilia ya Panguso sasa kiganjani kupitia Swahiliflix

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Tamthilia ya Kitanzania inayotikisa Afrika ya Panguso iliyowapa ajira wasanii 200 kuanza kuonyeshwa kiganjani mwako kupitia App ya Swahiliflix kuanzia Mei 1, mwaka huu baada ya mashabiki kuipenda na kuomba iendelee kuonyeshwa.

Akuzungumza na www.mtanzania.co.tz mapema leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Swahiliflix, Ibrahim Nassoro, amesema ni wakati wa Watanzania na Afrika kuangalia Panguso kiganjani mwao.

“Ni tamthilia nzuri na pendwa yenye maisha halisi ya kitanzania na mafunzo ya kutosha kwa wakubwa na watoto unaipata kupitia App ya Swahiliflix kwa Sh 1,000,” amesema Nassoro.

Nae, muandaaji wa tamthilia hiyo ambaye pia ni Msanii wa Filamu nchini, Jimmy Mafufu amesema kuwa ameweza kutoa ajira kwa wasanii 200 kupitia tamthilia hiyo na kusema kiwanda cha filamu wameweza kukifufua kwa upya.

“Niombe pia Serikali kuweza kutumia vizuri kiwanda cha Sanaa hasa filamu kwa kuwa ndio watu pekee wenye ushawishi katika jamii na kuacha kuwatumia kwenye kampeni zao pekee,” amesema Mafufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles