Yahoo imesema zaidi ya watu bilioni moja ambao ni watumiaji wa Yahoo wameathirika baada ya akaunti zao kudukuliwa mwaka 2013.
Imesema kuwa, hii ni takwimu mpya na tofauti na ile waliyoitoa September, 22, 2016 ambayo ilikuwa na takwimu ya akaunti zilizodukuliwa mwaka 2014 ambapo akaunti milioni 500 ziliathirika.
Yahoo imeeleza kuwa namba za simu, namba za siri na barua pepe viliibiwa lakini wadukuzi hawakugusa malipo ifa za benki.
Hata hivyo Yahoo inaendelea kufanya uchunguzi huku ikifanyakazi kwa karibu sana na polisi na mamlaka husika.
Yahoo imeendelea kusisitiza kuwa udukuzi huo ambao umedumu wa miaka mitatu, ni sehemu ya upelelezi uliokuwa ukifanywa na mamlaka pia wataalamu wa maswala ya ulinzi.
Kwakuwepo kwa swala hili, Yahoo imewasihi watumiaji wake kujitahidi kubadilisha namba zao za siri kwa usalama wa taarifa zao.
Kampuni hiyo kubwa iliyoko mjini California ina watumiaji ‘active’ zaidi ya bilioni moja kwa mwezi japokuwa wengine wengi wana akaunti zaidi ya moja. Zipo chache pia ambazo hazitumiwi mara kwa mara.