Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), inamshikilia kwa mahojiano Mmiliki wa Kampuni ya White Star Investment ya Dar es salaam,Taalib Mbowe kwa makosa ya ukwepaji kodi,udanganyifu na utakatishaji wa fedha.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dodoma jana na Takukuru na kusainiwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo,Doreen Kapwani ilisema Mbowe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya White Star Investment inayofanya biashara ya usafirishaji ndani na nje ya nchi kwa kutumia malori.
Taarifa hiyo, ilisema Mbowe anafanyiwa uchunguzi kwa makosa ya ukwepaji kodi,udanganyifu na utakatishaji wa fedha.
Pamoja na uchunguzi huo,taasisi hiyo inachunguza umiliki wa vichwa vya magari(treller) zaidi ya 100 zinazomilikiwa na mfaanyabishara huyo na mikopo yake ya zaidi ya zaidi ya Sh bilioni 6.3 kutoka benki za Barclays na Equity.
“Uchunguzi huu ukikamilika nakudhibitishwa tuhuma hizi, atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani,” ilisema taarifa hiyo.