30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara adakwa Takukuru

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU), inamshikilia kwa mahojiano Mmiliki wa Kampuni ya White Star Investment ya Dar es salaam,Taalib  Mbowe kwa makosa ya ukwepaji kodi,udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dodoma jana na Takukuru na  kusainiwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo,Doreen Kapwani ilisema Mbowe ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya White  Star Investment inayofanya biashara ya usafirishaji ndani na nje ya nchi kwa kutumia malori.

Taarifa hiyo, ilisema Mbowe anafanyiwa uchunguzi kwa makosa ya  ukwepaji kodi,udanganyifu na utakatishaji wa fedha.

Pamoja na uchunguzi huo,taasisi hiyo inachunguza umiliki wa vichwa vya magari(treller) zaidi ya 100 zinazomilikiwa na mfaanyabishara huyo na mikopo yake ya zaidi ya zaidi ya Sh  bilioni 6.3 kutoka benki za Barclays na Equity.

“Uchunguzi huu ukikamilika nakudhibitishwa tuhuma hizi, atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles