24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Taifa Stars ‘yapunguza’ gharama za matibabu JKCI

TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) imetoa punguzo la chini ya asilimia 50 kwa vipimo vya moyo kwa saa sita baada ya ushindi wa Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa Uhusiano wa JKCI, Anna Nkinda amesema huduma hiyo imetolewa kwa wagonjwa ambao hawana rufaa ya kwenda hospitalini hapo.

Amesema moja ya kipimo kilichotolewa ni kuangalia moyo unavyofanyakazi (ECHO) na umeme wa moyo (ECG).

“Jumla ya vipimo vyote pamoja na kumwona Daktari bingwa ni Sh 120,000 lakini katika punguzo hili atalipa 25,000,” amesema Anna.

Amesema kawaida kipimo cha ECHO hugharimu Sh 30,000 na kupima jinsi moyo unavyofanyakazi ni Sh 50,000 kumwona Daktari ni Sh 40,000 jumla 120,000.

Naye Mkurugenzi wa tiba shirikishi Delila Kimambo amesema katika vipimo hivyo waliofika hapo wamefanikiwa kuzungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka katika taasisi hiyo.

“Niiombe jamii kuhakikisha inapata matibabu sahihi kutoka katika taasisi sahihi na kuepuka vipimo visivyo na uhakika kwani JKCI tuna vipimo hivyo,” amesema Dk Delilla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles