27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Taharuki ya wanyama wakali yaendelea kuwa tishio kwa wakazi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro

NA Mwandishi wetu

Wananchi wa tarafa ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro wameendelea kuishi maisha magumu kutokana na Kushambuliwa na wanyama wakali kufuatia matukio yanayoendelea kutokea katika eneo hilo.

Afisa tarafa wa eneo hilo bwana Bahati Mfungo amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali imekuwa ni ya kutisha.

Katika matukio ya hivi karibuni zaidi ya matukio mawili yameripotiwa kutokea kwa wananchi na mifugo kupoteza maisha au kujeruhiwa vibaya katika tarafa hiyo.

Mwananchi anayejulikana kwa jina la Orkendenye Liarite mwenye umri wa miaka 32 kutoka kijiji cha Bulati akiwa machungani alishambuliwa na simba ambapo alijeruhiwa vibaya huku ng’ombe wake wawili wakiuliwa na simba huyo.

Mwananchi huyo amejeruhiwa ubavu wa kulia na usoni na kulazimika kukimbizwa haraka katika kituo cha afya cha Nainokanoka kwa ajili ya matibabu.

Katika tukio lingine mwananchi anayeitwa Kimirei Kuya mwenye umri wa miaka 26 alivamiwa na kiboko ndani ya nyumba yake ambapo katika hali isiyo ya kawaida alishambuliwa vibaya mwilini.

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Esere kata ya Alaitole ambapo mwananchi huyo alivamiwa na mnyama huyo na kuuawa.

Kufuatia matukio haya serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inaendelea kutoa elimu,kuhamasisha , kuandikisha, kuthaminisha na kuhamisha wananchi ambao wanataka kuhama kwa hiyari ili kunusuru maisha ya watu hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles