27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yazindua warsha ya watekelezaji wa Afua za Ukimwi

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), imezindua warsha ya siku moja ya Watekelezaji wa Afua za UKIMWI kwa fedha za mzunguko wa kwanza wa mfuko wa Kili Challenge.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo uliofanyika leo Januari 26, mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema kuwa dhima ya Kiliamanjaro Challenge Against HIV/AIDS katika historia ya mapambano dhidi ya Ukwimwi nchini ni kushirikisha wadau kuchangia kwa hali na mali mwitikoo wa Taifa  dhidi ya ugonjwa hauo.

Dk. Maboko amesema katika mzunguko wa kwanza wa programu hiyo mfuko umeweza kusaidia Asasi za kiraia 20.

“Katika mzunguko wa kwanza wa programu hii mfuko umeweza kusaidia Asasi za kiraia 20 ambazo zinapatiwa jumla ya Sh milioni 543.6 zikijumhisha mikoa 11 na Halmashauri 15 zinatarajiwa kunufaika kwenye awamu hiyo ya utekelezaji.

“Aidha, katika awamu hiyo ya kwanza maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na huduma na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU, huduma za kinga, elimuya masuala ya afya kwa vijana.

“Pia kuna misaada kwa watoto walio katika mazingira magumu, kupambana na unyanyapaa na ubaguzi, kutoa elimu kwa watoa huduma majumbani na elimu ya matumizi sahihi ya dawa za kufubaza VVU miongoni mwa waviu,” amesema Dk. Maboko.

Sehemu ya Washiriki wa Warsha hiyo

Amesema kwa Mkoa wa Geita programu hii imewezesha Kituo cha watoto yatima (Moyo wa Huruma) kuendelea kulea na kusomesha watoto yatima walioachwa na wazazi wao kutokana na janga hili la Ukimwi.

Pia katika Mkoa wa Arusha kikundi cha kina Mama wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa (Arusha Pastoral Women Counsel) wameweza kuboresha shughuli zao za ufugaji kupitia progamu hii, ambapo kwa sasa wanafuga kwa njia ya kisasa ambayo imepelekea kupata mapato makubwa ikilinganishwa na awali.

“Aidha, programu hii imeongeza weledi uelewa wa wananchi katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Asasi katika Mikoa ya Lindi, Kagera, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Kagera, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Pwani, Dar es Salaam na Kilimanjaro.

“Mfumo huu wa utoaji fedha kwa kuzishindanisha Asasi mbalimbali kutokana na ubora wa maandiko ndiyo umeanza kwa mzunguko wa kwanza ambapo Asasi hizi 20 zimeandaa mandiko bora zaidi miongoni ma waombaji 264 waliowasilisha maandko.

“Jambo la msingi hapa ni kuongeza uwazi na ubora wa maandiko ambapo matarajio ya Serikali kupitia TACAIDS na GGM ni kuona taasisi zilizopewa fedha zinatekeleza kwa ufanisi nakuhakikisha fedha zinawafikia walengwa huku malengo yaliyokusudiwa yakifikiwa,” amesema Dk. Maboko.

Aidha, Dk. Maboko ameongeza kuwa: “Malengo makubwa ya mpango mkakati wa kitaifa wakudhibiti UKIMWI wa awamu ya nne ni kuiwezesha serikali kuimatisha programu za kuzuia maambukizi mapya, kutoa huduma za tiba ya magonjwa nyemelezi, kupunguza athari za ugonjwa wa UKIMWI kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

“Pia kujenga mazingira bora ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia  maambukizo mapya ya VVU nchani ikiwa ni pamoja na yale ya kutoka kwa mama kwenda kwa rntoto pamoja na kupunguza maambukizo kwa wasichana balee na wanawake nchini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles