23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

TAASISI YAOMBWA KUBAINISHA VIUATILIFU VISIVYO NA MADHARA

 

 

JUDITH NYANGE

TAASISI ya Utafiti  na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania  (TPRI) imeshauriwa kubainisha dawa ya kuuwa wadudu wa mazao ambayo  haina madhara kwa binadamu.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mbegu  za Mazao ya  Kibo, Francis Chenge, alisema hatua hiyo itawaqwezesha  wakulima   kuitumia  ikizingatiwa wengi hawana elimu ya matumizi sahihi  dawa hizo.

Pia  aliitaka TPRI   a kuwa makini na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika mikoa ya pembezoni mwa nchi.

Alisema zipo  baadhi ya dawa za kuua wadudu ambazo hazijakaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika lakini  huingizwa nchini kwa njia za  magendo na kusababisha madhara kwa binadamu.

Alikuwa akizungumza kwenye maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa  yaliyomalzika juzi katika viwanja vya Nyamong’holo wilayani Ilemela,  Mwanza.

Chenge  alisema baadhi ya dawa za kuua wadudu wamazao zinaweza kuchangia   magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani hivyo ni vema TPRI ikabainisha dawa ambazo hazina madhara kwa binadamu.

Alisema ni vizuri pia kampuni za kutengeneza dawa zisizo na madhara kwa binadamu  ambazo mkulima atakaa muda mfupi baada ya kupuliza kwenye  mazao yake    aweze  kuvuna kutumia mazao yake  kwa chakula au kuyapeleka sokoni .

“Kuna baadhi ya dawa mkulima anatakiwa kukaa saa 24,  siku saba au hata mwezi mmoja baada ya kupuliza kwenye mazao   aweze kuyatumia kwa chakula na kusiwepo na athari zozote.

“Wakulima wengi hawana elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa hivyo nashauri dawa zenye madhara  na zisizo na madhara kwa binadamu zibainishwe ili tahadhari ichukuliwe,” alisema Chenge.

Mkulima  kutoka Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Emmanuel Mgeta,  alisema  dawa za kuua  wadudu wa mazao zina utaratibu  wa matumizi yake na mara nyingi huwa zinaandikwa   mtumiaji asome maelekezo ya matumizi yake  anapoitumia itumie kwa usahihi.

Alisema baadhi yawafanyabiashara huwauzia wakulima dawa ambazo si sahihi kwa    kuhitaji tu kuuza kwa sababu amekaa nayo muda mrefu sokoni.

Alisema  dawa kama hiyo inaweza kupulizwa kwenye mazao na kuua hata wale wadudu ambao  rafiki wa zao husika badala ya wale waharibifu.

Mgeta alisema  changamoto iliyopo ni wauzaji wengi wa pembejeo za kilimo kutokuwa na uelewa kuhusu  dawa wanazoziuza.

Mara nyingi  wengine hawana utaalamu   kuhusu biashara hiyo na kushindwa kabisa kumpatia mteja maelekezo  anaponunua bidhaa, alisema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles