25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi yahamasisha elimu kwa jamii

Ashura Kazinja, Morogoro

KUTOKANA na mwamko wa elimu kwa jamii mdogo, taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na Haki za Mtoto, Afya na Elimu (HACOCA), imefanya bonanza kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa elimu.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Mafiga,Manispaa ya Morogoro, Mratibu wa Mradi wa  HACOCA, Happiness Mshana alisema bonanza hilo ni maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa jamii juu ya umuhimu wa elimu.

Alisema mbali na Serikali kutilia mkazo juu ya elimu, bado mwamko wa jamii juu ya umuhimu wa elimu ni mdogo, ambapo wazazi wamekuwa hawana muda wa kufatilia maendeleo ya watoto wao shuleni au hata majumbani ili kumwezesha  kupata kile alichokusudiwa kukipata.

Aliwaomba baadhi ya wazazi ambao hawana utaratibu wa kuwapangia watoto wao majukumu wawapo nyumbani hasa kwa mtoto wa kike, kuanza utaratibu huo ili kuwawezesha kupata muda wa kutosha kujisomea, kufanya kazi walizopewa shule na kucheza.

“Mwamko wa jamii juu ya elimu bado ni mdogo, mtoto anashindwa kufika shule bila sababu wala mzazi hafuatilii maendeleo yake, hatuna utaratibu wa kuwapangia majukumu watoto wetu ili wapate muda wa kucheza na kujisomea, na wa kusaidia majukumu mengine madogo madogo ya nyumbani” alisema Mshana.

Alikemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachia watoto wao wa kike majukumu ya kulea wadogo zao, huku wao wakienda kwenye shughuli zao, ikiwemo vikoba na kumnyima mtoto hasa wa kike nafasi na haki ya kucheza, kwani mtoto anajikuta ana majukumu mazito kama ya mtu mzima.

Ofisa Maendeleo Kata ya Mafiga, Nesphora Kinoge, alipongeza jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo katika jamii, ikiwamo kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira hatarishi.

Ofisa Miradi Shirika la ‘Save The Future Foundation” (STFF), Isack Wilson alisema njia ya kutumia michezo kutoa elimu ni nzuri kutokana na watoto wengine kutopenda kwenda shule au walikosa elimu hiyo hapo awali na hivyo kupitia michezo mbalimbali wanaweza kujifunza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles