27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya TSO yajitosa kusaidia watoto yatima

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzanite Support Organization (TSO), imejitosa kusaidia vijana wanalolelewa katika vituo vya watoto yatima jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Support Organization (TSO), Bahati Chando(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa taasisi yake inayojiusisha na masuala ya kusaidia vijana.

Afisa Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bahati Chando amesema taasisi yao imeanzishwa kwa lengo la kutaka kusaidia vijana katika masuala ya Elimu, Afya na kiuchumi kwa kushirikiana wadau wa maendeleo.

‘tumeona vijana wengi hasa wanaoishi katika mazingira magumu wanavyopata shida nyingi kwa kukosa msaada, sisi tukaona tuanzishe taasisi itayosaidiana na wadau wa maendeleo kujaribu kutatua changamoto zao za kimaisha zinazowakabiri vijana’alisema.

Pia tuaomba wadau mbalimbali wajitokeze kuweza kusaidiana nasi kutatua changamoto vijana.

Afisa Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya Kinondoni, Neema Mwalubilo, akizungumza baada ya kuzindua Taasisi ya Tanzanite Support Organization (TSO) inayojihusisha na masuala ya kusaidia vijana wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima, kielimu, afya na uchumi, jijini Dar es Salaam leo Septemba 12.
Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mind Garden Psychological, Sumaiya Mohmoud, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Tanzanite Support Organization (TSO) inayojihusisha na masuala ya kusaidia vijana wanaolelewa katika vituo vya watoto yatima, kielimu, afya na uchumi, uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Vijana wanaolelewa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima jijini Dar es Salaam wakisilikiza hotuba za viongozi wakati uzinduzi wa Taasisi ya Tanzanite Support Organization (TSO).
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles