29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya TASMAP yazindua ‘Mama ndiye Mlezi wa Nyumba yetu Tanzania’

Na Brighiter Masaki,Dar es Salaam

Taasisi isiyo ya Kiserikali Tasmap, imezindua mradi wa Mama ndiye Mlezi wa Nyumba yetu Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango na ukombozi wa mwanamke katika jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Jumanne Juni 29, 2021 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Salum Kaporo, amesema tukio hilo litazinduliwa rasmi Julai 21 mkoani Ruvuma, huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dorothy Gwajima.

“Lengo ni kutoa elimu kwa akina mama, ya magonjwa mbalimbali ya jinsia na watoto katika kutoa elimu na kusaidia kuweza kumsaidia mama na kumkomboa mwanamke katika dunia ya sasa,” amesema Kaporo.

Kwa upande wake Diwani Viti Maalumu, Grace Betuel, amesema kuwa Kongamano hilo linatakiwa kuwasaidia wanawake kujua nafasi zao kwenye jamii na kutunza familia zao.

“Lengo ni kutaka Mwanamke atambue umuhimu na nafasi yake na kusaidia familia jamii na taifa ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kina mama katika familia zao,” amesema Grace.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles