26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Taasisi ya Moyo MNH yapungukiwa madaktari

Profesa Mohamed Janabi
Profesa Mohamed Janabi

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

LICHA ya kufanikiwa kufanya upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo nchini na kuokoa fedha nyingi za Serikali, Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inakabiliwa na upungufu wa madaktari kwa kiwango cha asilimia 50.

Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alieleza hayo jana mbele ya Balozi wa Israel nchini, Yahel Vilan Mar alipotembelea taasisi hiyo.

“JKCI tumefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo tangu mwaka jana taasisi ilipoanzishwa hadi hii leo, zaidi ya asilimia 80 ya wagonjwa tuliowahudumia ni watoto, kwa mwaka huu pekee tumeweza kuwahudumia watoto wapatao 604 na Israel imekuwa ikitupa ufadhili,” alisema.

Alisema Israel imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa taasisi hiyo hasa kwa upande wa kuwajengea uwezo madaktari, wauguzi na wataalamu wengine.

“Wametusaidia kusomesha madaktari sita hadi sasa ambao huenda moja kwa moja Israel kujifunza na bado wataalamu wao wamekuwa wakija nchini kutoa mafunzo kwa hawa wanaobakia nchini kwa mafunzo mafupi,” alisema.

Kwa upande wake Balozi wa Israel,  Yahel Vilan mar alisema Israel itaendelea kutoa msaada kwa Serikali ya Tanzania kwa kusomesha madaktari wengi zaidi wa taasisi hiyo ili iendelee kutoa huduma bora kwa ufanisi.

“Nimefurahi kuona kwamba mnafanya kazi nzuri ya kusaidia kuokoa maisha ya watu. Israel hatuna bajeti kubwa ya kuweza kuchangia mengi lakini nawaahidi kwamba tutahakikisha tunasaidia kutoa mafunzo na vifaa pale itakapowezekana kwa taasisi hii, bado tunayo nafasi ya kuendelea kusaidia Tanzania,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles