26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Steve Nyerere atoa neno kuhusu tozo

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Kikundi cha hamasa cha “Mama Ongea na Mwanao”, Steven Mengere maarufu kama, Steve Nyerere amesema viongozi wa siasa waache kubeza tozo zinazokatwa kwa maendeleo ya Taifa.

Steve ameyasema hayo leo Dar es Salaam Septmba 6, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amebainisha kuwa kumekuwepo na minong’ono isiyo na tija kwa malengo ya kubeza juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupigania kuwapo kwa tozo hizo ili kuleta mabadiliko na maendeleo ya nchi kupitia jasho la Watanzania pasipo kutegemea misaada kutoka mataifa mengine.

“Tumechoka kuwa masikini kila muda tunaomba misaada nchi zingine Taifa linaingia kwenye madeni kila kukicha na kusababisha maendeleo kutopatikana kwa wakati hivyo tozo hizi ni sahihi kuwepo ili kusaidia maendeleo kufanyika kwa wakati kwa kutumia pesa za Watanzania wa matabaka yote bila kujali wenye nacho na wasio nacho,” amesema Steve.

Steve pia amewahusia Watanzania kuwa sauti ya wengi ni sauti ya umoja, hivyo ni vyema kupeleka malalamiko kwa serikali ili yaweze kupitiwa upya endapo kutoanonekana tozo hizo ni kubwa sana hasa kwenye makato kuliko kupigia kelele kufutwa kwa tozo kabisa.

Pia amewaomba viongozi kuweka utabaka wa vyama vyao linapokuja swala la nchi kuhitaji maendeleo yake pasipo mikopo ya nje na kuongeza kuwa siasa zisivunje nchi yenye kuhitaji maendeleo kupitia tozo za wananchi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles