27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Special Olympics Tanzania yaendesha mafunzo kwa walimu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Taasisi inayojihusisha na michezo kwa watu wenye ulemavu wa akili(Special Olympics Tanzania), inaendesha mafunzo kwa walimu kutoka Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutambua mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika kushiriki michezo jumuishi na wenzao.

Mtendaji Mkuu wa Special Olympics Tanzania, Charles Rays amesema mafunzo hayo yanayofanyika kituo cha michezo cha JMK Park, yanahusisha walimu 24, kutoka Kigamoni na wafanya kazi wa kituo hicho.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanaratibiwa na Kamati ya Olimpiki ya Ujerumani ambayo imeagiza mafunzo yafanyike ili watoto wenye ulemavu wa akili wafanye michezo pamoja na wenzao lakini baadae washindane wenyewe kwa wenyewe hadi ngazi ya mkoa, kisha kuchagua timu ya Taifa.

“Haya mafunzo yanafanyika katika nchi nne za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Burundi, Uganda na Kenya. Kwa Tanzania Dar es Salaam tumechagua Kigamboni, Morogoro tutafanya Mvomero, kisha jijini Dodoma na jijini Arusha,” amesema.

Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Mwalimu Jones Leonard kutoka shule ya msingi Buyuni, Kigamboni, amesema mafunzo hayo yamemsaidia kujifunza vitu ambayo alikuwa havifahamu kuhusu watoto wenye ulemavu wa akili.

“Kabla ya kufika hapa kuna vitu vingi nilikuwa sivifahamu juu ya hawa watoto wenye ulemavu wa akili, lakini jinsi mafunzo haya yanavyoendelea nitajifunza vingi na nikirudi kazini nitawafundisha vile wanavyotakiwa ili waweze kushiriki michezo na wajisikie kama watoto wengine ambao hawana matatizo,” ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles