26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

SOS wazindua kampeni kupinga ukatili kwa watoto

BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la SOS Children Villages kwa kushirikiana na Taasisi ya Amend na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, wamezindua kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watoto.

Akizungumza na MTANZANIA jana Dar es Sakaam wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika Chanika, Mkurugenzi wa Amend, Neema Swai alisema watatoa elimu ya usalama barabarani mashuleni ili kupima uelewa wa mtoto kutokana na jinsi alivyofundishwa.

“Kampeni yetu kwa mwaka huu imebeba kaulimbiu ya ‘kupinga ukatili dhidi ya watoto unakatisha ndoto zao, hivyo inapaswa tuwalinde, tuwatunze na tuwajali wanapotumia barabara’,” alisema.

Neema alisema wamegawa mradi huo makundi matatu ambayo mradi wa kuimarisha familia, mradi wa cheza na jifunze na mahakama ya watoto.

“Katika kuimarisha familia, mtoto atapewa elimu ili kuelimisha familia yake kwa haraka zaidi, cheza na kujifunza wanafunzi watashindanishwa kuchora picha zinazoonyesha matukio yanayofanyika barabarani, na mahakama ya watoto madereva watakaokuwa na makosa watakamatwa na kupelekwa kwenye mahakama na kuhojiwa kutokana na makosa yao ili kusaidia kuwalinda watoto,” alisema Neema.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Chanika, Frank Malogwa, alisema wanashukuru kuwepo kwa kampeni hii inayohamasisha malezi na mafunzo ya usalama kwa watoto kwenye ngazi ya kifamilia pamoja na wananchi kwa ujumla

Mratibu wa Polisi Usalama Barabarani, Abel Swai alisema suala la elimu ya usalama barabarani linahitajika kwa watu wote ili kuepukana na ajali, huku akiwataka vijana kufuata sheria za barabani. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles