25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wawili NEMC waondolewa Bandari Dar

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene, ameagiza kuondolewa kwa wakaguzi wawili wa Baraza la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), waliopo Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu suala la vifungashio vya plastiki vinavyokuja na bidhaa mbalimbali kutoka nje.

Uamuzi huo aliutangaza juzi mbele ya waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es Salaam.

Simbachawene alisema kumekuwa na changamoto nyingi, ikiwemo suala la vifungashio na mifuko mbadala licha ya kanuni kuwa wazi.

Pia alibainisha vifungashio vya plastiki zinavyoruhusiwa na visivyoruhusiwa.

“Kanuni ya 9 imebainisha vifungashio vya plastiki vinavyoruhusiwa ni ile vinavyotumika kwa ajili ya huduma za afya, bidhaa za viwandani, sekta ya ujenzi, sekta ya kilimo, vyakula, usafi na udhibiti wa taka.

“Mnakwamisha biashara za watu, hasa hawa wanaoingiza bidhaa za viwandani kama nguo.

“Ukishaondoa kifungashio kwenye nguo, mpaka ifike dukani kutoka bandari itakuwa nguo kweli?” alisema na kuhoji Simbachawene.

Mbali ya agizo hilo, pia alisema mkanganyiko huo unatokea kutokana na watumishi kukosa weledi wa taaluma au kazi wanazofanya na kusababisha kufanya kazi kwa kubahatisha na kukosa ufanisi katika utendaji kazi wao na kuchangia usumbufu, hasa kwa wafanyabishara wanaoingiza bidhaa mbalimbali za viwandani nchini kutoka nje.

Aidha, Simbachawene aliagiza watumishi kutoka NEMC Kitengo cha Ukaguzi Bandarini kufanya kazi saa 24 wakishirikiana na watumishi kutoka taasisi nyingine za Serikali ili kuongeza nguvu kazi katika ukaguzi wa mizigo inayoingia nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles