30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Soko la Samaki Katemba lawanufaisha wananchi Muleba

Renatha Kipaka, Muleba

Soko la Samaki na Dagaa Katembe-Magarini limeanza kuwapa manufaa Wananchi wilayani Muleba mkoani Kagera.

Aidha, soko hilo limesaidia kuinunua uchumi wawananchi wanaoishi katika Kijiji cha Katembe Kata ya Nyakabango katika mwalo wa Katembe Magarini kwa kuuza

bidhaa za madukani, ubebaji wa mizigo pamoja na mama lishe.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amewashauri wafanyabiash

ara kulitumia soko hilo kwa ajili ya kusafirisha samaki na dagaa kwenda sehemu mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Amesema ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wafanyabiashara wanaendesha biashara zao katika mazingira bora na salama ambayo yatawawezesha wao na serikali kupata faida.

“Hapa hatuna vikwazo vyovyote kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa kwenda nje na wafanyabiashara wa ndani gharama ni ndogo ukilinganisha na gharama ambazo zinatozwa kwenye mialo mingine,”amesema Nguvila.

Kwa upande wake Afisa Uvuvi wa wilaya, Wilfred Tibendelana ameeleza kuwa kwa sasa wananchi wa eneo la mwalo wa Katembe tayari wameshaanza kunufaika na soko la dagaa na samaki na wakati huohuo kuwezesha serikali kuu na Halmashauri kupata mapato.

Ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara wote waliopo ndani na nje ya wilaya ya Muleba kuendelea kulitumia soko hilo la Katembe-Magarini kwani tozo zake ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine.

Pia msimamizi Mkuu wa Bandari ya Katembe-Magarini, Sande Ruben Mtambo ametoa takwimu na kusema kuwa tangu mizigo ya dagaa ianze kushushwa kupitia bandari ya Katembe-Magarini mpaka sasa zimeshushwa tani 13,033.95 na mapato yameongezeka kwa wastani wa kutoka milioni 13 hadi kufikia milioni 16 kwa mwezi mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles