25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Sirro: Hatutabweteka kupatikana kwa Mo

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam



Baada ya kupatikana kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa Klabu ya Simba, bilionea Mohamed Dewji maarufu Mo, aliyetekwa wiki iliyopita katika Hoteli ya Colloseum, jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi nchini limesema halijaridhika, litaendelea kuwasaka waliotekeleza tukio hilo.

Mo alipatikana usiku wa kuamkia leo, akiwa ametelekezwa na gari linalodaiwa kuhusika kumteka siku ya tukio, katika Viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio leo Jumamosi Oktoba 20, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)Simon Sirro amesema jeshi lake kwa kushirikiana na Interpol, linaendelea kuwasaka watu hao hadi wapatikane.

“Miongoni mwa waliomteka Mo Dewji, yumo Mtanzania, kwa wale wengine tayari makachero wameshapelekwa katika nchi husika ili kuwakamata watu wanaohusika kufanya tukio hilo.

“Wananchi waendelee kutoa ushirikiano, kwani watu hawa wameanza kwa Mo, watafanya kwa mtu mwingine, kwa hiyo kuacha hizi silaha na kutelekeza gari hapa si mwisho, wa biashara hii ni lazima tuonyeshe hii ni Tanzania, lazima tuwapate,” amesema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro amesema kwa mujibu wa Mo, watekaji walikuwa wanazungumza lugha ya Kingereza na Kiswahili kwa mbali na amezitaja silaha zilizokutwa katika gari lililomtelekeza mfanyabiashara kuwa ni bunduki AK 47 na bastola tatu zenye risasi 19.

“Kama nilivyowaeleza jana na kuwaonesha picha ya gari lililomteka Mo tukio halisi mmeliona  gari ni lile lile Surf na kiukweli wangechelewa kumwachia ningewakamata na kuwakamata kwangu kungekuwa kwa aina,” amesema.

Aidha IGP Sirro amewataka wananchi  kuachana na habari za mitandaoni kwani  lengo lake ni  kupotosha umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles