23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Siri zavuja kuuawa Khashoggi

LONDON, UINGEREZA

KIFO cha mwandishi wa habari mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, kimezidi kuibua mambo mazito ambayo yamesababisha mauti yake.

Taarifa zinasema kuwa Khashoggi aliuawa baada ya kufichua kuwa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia unafadhili kituo cha televisheni ambacho kimekuwa kikitumika kuipinga na kuikosoa Serikali ya Iran ambapo inarusha matangazo yake kutoka Uingereza.

Kwa mujibu wa ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa mwandishi wa gazeti la The Guardian nchini Uingereza, Saeed Kamali Dehghan, kupitia mtandao wa Twitter, amesema katika makala iliyochapishwa Oktoba 2 mwaka huu na Guardian, alinukuu duru za karibu na utawala wa Saudia ambazo zilimdokezea kuwa, Televisheni ya Iran International, hupokea msaada wa dola milioni 250 kutoka Saudia kila mwaka.

Khashoggi aliuawa kinyama siku hiyo ambayo gazeti hilo lilichapisha ripoti hiyo. Baada ya mauaji hayo, gazeti la The Guardian, liliandika kuwa Televisheni ya Iran International inafadhiliwa na mfanyabiashara Msaudia, Saud al-Qahtani, ambaye ni mpambe na mshauri wa mrithi wa kiti cha ufalme, Mohammad Bin Salman.

Al-Qahtani ni kati ya maofisa wa ngazi za juu wanaodaiwa kutimuliwa na Bin Salman baada ya kuuawa Khashoggi ili kupunguza mashinikizo ya kimataifa.

Baadhi ya duru zinasema al-Qahtani ni miongoni mwa wapambe wa Bin Salman waliosimamia na kuelekeza mauaji ya Khashoggi.

Imedokezwa kuwa al-Qahtani aliongoza mauaji hayo kwa njia ya video kupitia Skype ambapo aliamuru wauaji wampelekee kichwa cha Khashoggi.

Khashoggi, aliuawa Oktoba 2 mwaka huu baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul nchini Uturuki.

Hadi sasa mwili wa Khashoggi haujapatikana na wakuu wa Uturuki wanasema wana ushahidi kuwa mwili wake uliyeyushwa kikamilifu kwa asidi.

Serikali ya Uturuki imesema inaendelea na uchunguzi wa mauaji ya Khashoggi na kwamba itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu ukatili huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles