21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Simbachawene aridhishwa na miradi ya WHI

*Asema Serikali itaiongezea mtaji zaidi na kufikia watumishi wengi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameipongeza Taasisi ya Nyumba ya Watumishi Housing Investment(WHI) kwa namna ambavyo imeweza kupiga hatua ndani ya muda mfupi.

Waziri George Simbachawene akizunguma na Waandishi wa Habari.

Simbachawene ametoa pongezi hizo leo Mei 6, 2023 baada ya kutembelea moja ya mradi unaotekeleza na WHI uliopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa taasisi hiyo inafanya kazi kubwa licha ya changamoto yake ya mtaji kuwa mdogo.

Amesema kuwa pamoja na jitahada hizo Serikali itaangalia namna ya kuiongezea mtaji taasisi hiyo ili kuweza kuwafikia watumishi wengi zaidi hususan walioko pembezoni.

“Taasisi hii ya WHI haina muda mrefu tangu kuanzishwa kwake lakini imefanya kazi nzuri ambayo imesaidia watumishi zaidi ya 900 kupata makazi bora na kwa gharama nafuu, hii ni hatua kubwa kwani pamoja na mtaji wao kutokuwa mkubwa wakini wameweza kufanya kazi nzuri na kupunguza machungu ya makazi kwa watumishi wa umma.

“Serikali tutaangalia namna ya kuiongezea mtaji WHI kupitia bajeti ili iweze kufika maeneo mengi zaidi nchini na kuwafikia watumishi walio wengi,” amesema Simbachawene.

Amesema kuwa watumishi hawako katika maeneo ya mijini tu bali hata vijijini wapo na hivyo kuisisitiza WHI kutekeleza miradi yake katika maeneo mbalimbali.

“Watumishi hawako Dar es Salaam tu, Dodoma au Mwanza bali wapo mijini na vijijini katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo tungependa kuona hata maeneo ya pembezoni mwalimu anaishi katika nyumba bora iliyojengwa na WHI kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake akiwa na makazi bora,” amesema Simbachawene.

Simbachawene ameongeza kuwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida Fund kutasaidia taasisi hiyo kutunisha mtaji wake na kuipa nguvu ya kutekeleza miradi mingi zaidi na ya gharama nafuu zitakazoweza kupangwa au kununuliwa na watumishi wa umma.

Dk. Fredy Msemwa.

Upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa WHI, Dk. Fredy Msemwa amesema kuwa wamepokea maelekezo ya kutanua shughuli zao nchi nzima na kwamba watalifanyia kazi.

“Jambo la kutanua shughuli zetu litahitaji kuwa na mtaji mkubwa ambapo Waziri ameahidi kuwa Serikali itaiongezea WHI mtaji kwa ajili ya kutekeleza azima hiyo.

“Kuhusu mwenendo wa Faida Fund unaendelea vizuri na sasa umefikisha Sh bilioni 15 na thamani ya vipande imeongezeka kutoka Sh 100 hadi Sh 103.42 kwa hiyo ni ukuaji mzuri ambao kwa mwaka tunaweza kufikia ukuaji mzuri wa zaidi ya asilimia 10 hadi 11, hivyo tutaendelea kuwawezesha watumishi wa umma kuwa na makazi bora kwa gharama nafuu,” amesema Dk. Msemwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles