25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Simba yatumiwa ujumbe wa kitisho

THERESIA GASPER-GASPER-DAR ES SALAAM

BAADA ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, Kocha Msaidizi wa Azam, Iddy Nassor ‘Cheche’,  ameitaka  Simba ijiandae kukutana na maumivu na kipigo kutoka kwao.

Azam na Simba zitashuka dimbani kuumana, katika pambao la Ligi Kuu Tanzania Bara, litakalopigwa Marchi 4 mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kauli ya kishujaa ya Cheche imekuja siku moja baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi huo dhidi ya JKT Tanzania, mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Cheche alisema haikuwa kazi rahisi kwao kupata pointi tatu ugenini, lakini kutokata tamaa kwa wachezaji wake na kupambana dakika zote tisini kumewasaidia waweze kutoka kifua mbele.

“Kwa sasa tunarejea nyumbani kujiandaa na mchezo unaofauata dhidi ya Simba, kwani mtoto atakuwa hatumwi dukani hivyo tutahakikisha hatuwapi tena nafasi Simba ya kutufunga kirahisi,” alisema.

Alisema katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, kuna baadhi ya makosa aliyabaini ambayo ataendelea kuyatafutia tiba ili yasijitokeze kwa mara nyingine.

Cheche alisema wataendelea kupambana na kutoruhusu makosa kama ilivyokuwa kwenye mechi za nyuma ambako walipata sare na kufungwa.

Alisema kwa sasa wanatizamia nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi hivyo usipokuwa makini unaweza ukapoteza na kushuka chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles