31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaita vyombo vya dola kuchunguza

Haji-Manara-SimbaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema upo radhi vyombo vya dola vichunguze mkataba wao na mchezaji, Ramadhani Singano ‘Messi’, ili kuweza kubaini ukweli na kutatua utata unaoendelea kwa sasa.
Messi atakuwa mchezaji wa pili Simba mkataba wake kuchunguzwa na vyombo vya dola baada ya ule wa Athuman Idd ‘Chuji’ kudaiwa kufojiwa saini kama lilivyo sakata la Messi, kipindi anataka kuihama klabu hiyo mwaka 2008/2009.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema vyombo hivyo pekee ndivyo vinavyoweza kulimaliza suala hilo na wapo tayari kwa wao kufika na kuchunguza.
“Kila mmoja amekuwa akizungumza yake, lakini ukweli sisi tunaendelea kumtambua kama bado ni mchezaji wetu, tuna mkataba naye wa mwaka mmoja lakini uthibitisho zaidi utaamuliwa na vyombo hivyo,” alisema.
Alisema licha ya kusubiri uhakika huo, lakini wapo tayari kwa tamko lolote kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuhusiana na hilo, kwani wao pia wanakopi ya mkataba huo.
“Tupo tayari kwa majibu yoyote tutakayopewa baada ya uchunguzi huo kukamilika, kwani tunataka kuona kila kitu kinafanyika kwa misingi ya haki,” alisema.
Alisema kitendo hicho cha Messi kimewasikitisha uongozi wote kwani si halali kwa yeye kulalamikia kitu ambacho si sahihi na hiyo ni kutokana na kuponzwa na wakala wake, huku wakishangazwa na mchezaji huyo kuwa na wakala wakati amekuzwa na kupandishwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kuhusiana na suala la yeye Msemaji kwenda nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya Cosafa kusaka wachezaji ambao watasajiliwa na timu hiyo, alisema wapo wachezaji ambao amewaona kutoka nchi mbalimbali na ameshafikisha suala hilo kwa uongozi.
“Ni mapema sana kwa sasa kusema nchi wanazotokea wachezaji hao, ila nimekamilisha hatua muhimu niliyotumwa na uongozi sasa kazi nimewaachia wao,” alisema.
Alisema kwa upande wa usajili wanaendelea na mchakato huo kwa kufuata maelekezo ya kocha Goran Kopunovic, ambapo pia taratibu za kupatikana kwa kocha mpya au Goran kuendelea na mkataba zitafahamika ndani ya siku tatu kuanzia sasa, huku wachezaji watakaotemwa watawekwa hadharani Ijumaa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles