27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Simba wapata matumaini ya ubingwa

5NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Klabu ya Simba umeanza kujivunia kuimarika kwa stamina ya wachezaji wao na kujiongezea uhakika wa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, baada ya kushindwa kunyakua taji hilo kwa misimu mitatu mfululizo.

Tatizo la kukosa stamina ni moja kati ya dosari zilizogunduliwa na kocha msaidizi wa timu hiyo, Mganda Jackson Mayanja, ambaye tangu akabidhiwe kikosi hicho amekutana na matatizo ya wachezaji kushindwa kuhimili dakika 90 za mchezo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema baada ya kocha kuanzisha programu ya wachezaji kufanya mazoezi ya gym asubuhi kabla ya kuendelea na mazoezi ya uwanjani, timu imeanza kuwa na mabadiliko makubwa.

“Tatizo hili sugu kwa wachezaji wa Simba limeanza kupotea kabisa hata ukiwaangalia katika mazoezi unagundua kuna kitu kipya wamekipata, pumzi imerudi, stamina imeongezeka mambo ambayo ni muhimu,” alisema.

Alisema kwa sasa hawana wasiwasi wa kupata ushindi na Simba ndio mabingwa wapya msimu huu, kwani hakuna kikwazo kinachoweza kukwamisha malengo yao kutokana na kikosi hicho kubadilika na kuwa imara.

Manara alisema timu hiyo inaendelea kufanya maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya African Sports ya Tanga unatarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kushuka dimbani mara 15, Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia pointi 33 nyuma ya vinara Yanga wanaoongoza kwa pointi 39 sawa na Azam FC waliopo nafasi ya pili wakitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles