29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Simba SC yazipigia hesabu Azam, Yanga

simbaTIMU ya Simba imeanza kufufua matumaini ya kuwania taji la Ligi Kuu

Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Ndanda FC bao 1-0 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini hapa.

Katika mchezo huo uliokuwa na upinzani wa aina yake, umeiwezesha Simba kuwakaribia Azam na Yanga walio juu katika msimamo wa ligi hiyo.
Katika mchezo huo Simba walikuwa wa kwanza kufika lango la Ndanda na dakika ya tatu Hamis Kiiza alipoteza nafasi ya kufunga.

Ndanda walijibu mapigo baada ya Salvatory Ntebe, kushindwa kufunga shuti la adhabu katika dakika ya nne.
Baadaye Ndanda walipata bao katika dakika ya nane kupitia kwa Atupile Green, lakini mwamuzi, Rajab Mrope kutoka Songea, alilikataa kwa kuwa tayari alikuwa ameotea.

Simba walipoteza nafasi ya kufunga katika dakika ya 16, baada ya Paul Kiongera kushindwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Brian Majwega.
Ndanda wangekuwa makini katika dakika ya 38 wangeweza kupata bao lakini shuti la Omary Mponda lilitoka nje.

Simba walikosa bao katika dakika ya 62 baada ya Kiiza kutaka kuunganisha kwa kichwa krosi ya Mohamed Hussein, lakini mpira uligonga mwamba.
Kiiza alipoteza nafasi nyingine ya kufunga katika dakika ya 73.
Lakini Ibrahim Ajibu aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kiongera aliipatia Simba bao katika dakika ya 85.
Hadi mchezo huo unamalizika Simba walitoka kifua mbele kwa bao hilo na hivyo kuzikaribia Azam na Yanga.
Simba kwa matokeo hayo imefikisha pointi 27 sawa na Mtibwa Sugar lakini Wekundu hao wa Msimbazi wanapanda hadi nafasi ya tatu kutokana na kuwa na mabao 20 ya kufunga.
Azam wao wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 35 huku Yanga wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 33.
Hatua hiyo inaashiria sasa timu hizo kongwe nchini zitakuwa zikichuana vikali kuwania ubingwa wa Tanzania Bara.
Ndanda: Jackson Chove, Aziz Sibo/Masud Ally, Ahmad Msumi, Hemed Koja, Salvator Ntebe, Jackoson Nkwera, Braison Raphael, Wilium Lucian, Omary Mponda, Atupele Green, Kig Makasi.
Simba: Vicent Angban, Emery Nimuobona, Mohamed Hussein, Abdul Banda, Jjuko Murshid, Justice Majabvi, Dany Lyanga, Mwinyi Kazimoto, Hamis Kiiza, Paul Kiongera/ Ibrahim Ajibu na Brian Majwega/Said Ndemla.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles