25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kukutana kusuka mipango

Winfrida Mtoi- Dar Es Salaam

BENCHI la Ufundi la Simba linatarajia kukutana na wachezaji wao wakati wowote kuanzia sasa, ili kuwapangia program maalum za kufanya kipindi hiki cha mapumziko.

Uongozi wa Simba ulitoa siku saba kwa wachezaji wao kuendelea na mazoezi binafsi wakiwa wajumbani na kupanga kukutana wiki hii lakini ilishindikana.

Simba kama zilivyo klabu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara iliwapa mapumziko wa wachezaji wake, baada ya Serikali kupiga marufuku kwa siku 30 shughuli zinazosababisha mikusanyiko, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona, ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

Baada ya tamko hilo baadhi ya makocha wanaofundisha timu mbalimbali katika ligi hiyo walitoa program maalum za mazoezi  kwa wachezaji wao na kutakiwa kuzifanya lakini uongozi wa Simba ilipanga kukutana baada ya siku saba ili kupanga nini cha kufanya katika kipondi hiki cha mapumziko.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola  alisema hawakuweza kukutana kama walivyopanga kutokana na  msiba wa Ofisa Habari wa zamani wa klabu yao, Asha Muhaji ambaye alifariki Jumatano wiki hii.

Matola alisema, wanatarajia kukutana wakati wowote kuanzia sasa na uongozi wa klabu hiyo ili kupata maelekezo ya kile wanachopaswa kufanya wakati huu ambao michezo imepigwa marufuku.

“Hatujakutana kama ilivyopangwa kwa sababu siku tuliyotarajia kufanya hivyo tulipatwa na msiba, sijajua ni lini tutakutana, hilo ni jukumu la uongozi,” alisema.

Kuhusu kuwafuatilia wachezaji wao kama  wanaenendelea na mazoezi huko waliko, alisema ni ngumu kile wanachokifanya huko majumbani kwao.

 “Kila mchezaji yupo nyumbani kwake, huwezi kumfuatilia, ni yeye mwenyewe anapaswa kujitambua, ajue nini anatakiwa kufanya ili kutunza kiwango chake,”alisema Matola.

Simba ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa imejikusanyika pointi 71, baada ya kushuka dimbani mara 29, ikishinda michezo 24, sare mbili na kuchapwa mara tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles