Katika nchi nyingi za dunia, Jumatano, tarehe nane mwezi wa Machi itakuwa kilele cha kusherehekea siku ya wanawake duniani. Tayari vikundi kadha wa kadha vishaanza kutenda matendo yanayodhihirisha tabia za utu na huruma wanazozifanya wanawake kwa jumla.
Wanawake wengi hawangojei siku ile watafanikiwa kwa njia kubwa ndio wakupe usaidizi maalum, iwe nyinyi ni wa ukoo mmoja au la. Usidhani kama mama fulani ashashiriki kwa bet with bet365 kwani aonyesha ukarimu mwingi.
Hii tabia ni tofauti na wanaume wengi ambao mara nyingi lazima uwape sababu kubwa kabisa ndio wakugawie walicho nacho, ama wakusaidie, kama wewe ni mgeni kwao.
Siku ya Wanawake Duniani Yaadhimishwa Nchini Tanzania
Hapa Afrika, vikundi mbalimbali vimekuwa vikishiriki shughuli kadha wa kadha, kwa minajili ya kuipa umaarufu siku hii inayowakumbusha watu duniani majukumu makubwa, ambayo wanawake wamejitwika ili kuboresha maisha ya jamii.
Wawekezaji hapa Tanzania hawajawachwa nyuma katika kuipa kipao mbele siku hii maalum. Siku ya Jumanne, tarehe saba mwezi wa Machi, kampuni ya kuchimba migodi nchini inayoitwa Barrick, iliandaaa misheni iliyohusisha baadhi ya wafanyi kazi wake wa kike, kuitembelea hospitali moja maalum mkoani Mwananyamala.
Hiki kikundi kiliwapasha wasimamizi wa hospitali hiyo ya rufaa vifaa maalum vya matibabu, kwa niaba ya kitengo cha kampuni ya Barrick kilichoko mjini Dar-es-salaam. Aliyekiongoza kikundi hicho cha wafanya kazi wa Barrick ni meneja wa mawasiliano katika kampuni hiyo nchini Tanzania, Georgia Mutagahywa, ambaye alisema kwamba kampuni yao huwa na miradi mbalimbali iliyoelekezwa kuinua maisha ya jamii.
Jumuia Ya Madola Inavyoadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Miongoni mwa zaidi ya nchi hamsini zilizo wanachama wa Jumuia ya Madola, ishirini na moja ziko katika bara la Afrika. Hivyo basi, ni jambo la kufurahisha kuona kwamba mwaka huu Jumuia ya Madola imekipa kipao mbele suala la elimu kwa wasichana.
Kuna kamati inayojadili suala hili, hapo ikitarajia kusherehekea hapo tarehe nane Machi, kazi muhimu ambazo wasichana na wamama wanaendelea kufanya duniani. Bila shaka, utaratibu huu ni wa muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, Kenya na Uganda, nchi ambazo zilitawaliwa na Uingereza hapo miaka ya hamsini.
Jumuia ya Madola ni mojawapo ya mashirika ambayo yazidi kusisitiza usawa wa kijinsia, washiriki wake wakijua na kutaja wazi kwamba, kiwango cha wanawake walioelimika ni kidogo mno duniani kikilinganishwa na wanaume. Bila shaka, wasioelimika na walio na kiwango duni cha elimu hawapati nafasi nzuri za kazi, na kiwango cha maisha yao huwa ni hafifu.
Hivyo basi, hapo Jumuia ya Madola ikiadhimisha siku ya wanawake duniani kirasmi huko Marlborough House, Uingereza, dhana kubwa litakuwa vile shirika hili linaweza kusaidia nchi nyingi kuelimisha wasichana wengi inavyowezekana. Hatimaye, lengo la Jumuiya ya Madola ni kuhakikisha ya kwamaba idadi ya wanawake wanaojumuishwa kwa vyeo mbalimbali vya uongozi imefikia asili mia thelathini katika nyanja zote za maisha.
Bila shaka kuna matumaini makubwa kwa wakati huu, kwani nchi za Afrika zishaanza kuthamini uongozi wa wanawake. Rais wa Jamuhuri ya Tanzania hii leo ni Bi Samia Suluhu Hassan, na hapo juzi, kwa miaka kumi na miwili hadi mwaka wa 2018, rais wa nchi ya Liberia alikuwa Bi Ellen Johnson Sirleaf.
Maendeleo mengine yanazidi kuonekana pia katika uwakilishi wa wanawake bungeni hapa Afrika. Ijapokuwa nchi nyingi hazijafikisha asilimia hamsini kama vile nchi ya Rwanda imefanya, nchi kama Tanzania na Kenya zimezidi kuongeza idadi ya wanawake wanaoshikilia yadhifa maalum, sio tu bungeni, lakini kwa mambo ya uongozi kwa jumla.