24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Siasa ‘chafu’ zinavyorudisha nyuma miradi ya maendeleo Iringa

Na Raymond Minja, Iringa

Maisha ni Siasa ndivyo wahenga wanavyosema, lakini ikitumika vibaya kwenye miradi ya meendeleo na ya kimkakati hubadilika na kuwa majanga .

Moja ya miradi iliyoleta mvutano wa kisiasa katika Manispaa ya Iringa ni pamoja Machinjio ya Ngelewala ulioanzishwa mwaka 2008 wakati mstahiki Meya akiwa, Amani Mwamwindi .

Andiko la mradi huo wa machinjio ulikuwa ni kujenga machinjio ya kisasa na itakayokidhi vigezo vya Kimataifa ili nyama zitakazochinjwa hapo ziweze kwenda Uarabuni na Ulaya.

Na hii ni kwa sababu nchi za Uarabuni kuwa jangwa na katika nchi zao hakuna mifugo, hivyo kulikuwa na uhitaji mkubwa wa nyama toka Afrika jambo ambalo lingeibua fursa nyingi kwa watu.

Makisio ya mradi huo wakati wa uongozi wa Mwamwindi ilikuwa mpaka kumalizia machinjio hayo itagharimu kiasi cha Sh bilion 2 na milion mia tano.

Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulimuondosha Meya huyo madarakani ni baada ya Chama cha Chadema kushinda kata 18 na kuunda Halmashauri ya Manisaa ya Iringa.

Hivyo, mpaka 2015 Mwamwindi anaondoka madarakani inasemekana mradi huo ulikuwa umeshatumia Sh milioni 800.

Badaa ya kutoka Meya Mwamwindi,kijiti chake kikapokelewa na aliyekuwa Mstahiki Meya kipindi hicho, Alex Kimbe ambaye hakudumu baada ya kupigwa zegwe .

Kimbe alisema kuwa Mwaka 2016 halmashauri ilipata ufadhili kutoka Shirika la (UNIDO) na kuwapatia vifaa vyote vinavyohusika na kusindika minofu pamoja na mashine za kuhifadhia nyama.

“Tulipewa vifaa vingi vinavyotumika katika machinjio ya kisasa hii ikiwa ni pamoja na mitambo mikubwa miwili, majokovu kwa ajili ya kutunza nyama kabla hazijasafirishwa kwenda nje.

“Gharama za mradi huu zilikuwa ni wastani Sh milioni 300 na tulipewa vifaa hatukupewa fedha,” amesema Kimbe.

Anasema Mwaka 2017 kwa kutumia mapato ya ndani Manispaa hiyo ilifanikiwa kuweka mfumo wote wa umeme mkubwa wa viwandani kwenye machinjio na kagharamia kununua transifoma na walitumia Sh milioni 162.

“Mwaka 2018 wataam wetu wa manispaa waliandika andiko serikalini namna ya machinjio hayo yatakavyoinufaisha manispaa pamoja na mikoa inayozunguka Iringa.

“Baada ya kuandaa andiko hilo serikalini ilituma wataalamu kwenda kufanya ziara Ngelewala na baadae Waziri wa Tamisemi wakati huo (Suleman Jafo) akafanya ziara na kufurahishwa na mradi huo.

Kimbe anasema mwaka 2019 Serikali iliwapatia fefha Sh bilioni 1.1 kwa ajili ya kumalizia kazi zote zilizokuwa zimebakia kwenye machinjio hayo.

“Mwaka 2019 mimi nikiwa meya na Mkurugenzi akiwa Njovu tuliitwa Dodoma na katibu Mkuu Wizara wa Fedha na Mipango wakati huo(Doto James) huku naibu Katibu Mkuu TAMISEMI akiwa Dk. Dorothy Gwajima, tulisaini mkataba wa kupokea hizo fedha kwa ajili ya kumalizia kazi zote zilizokuwaa zimebaki,” anasema.

Anasema kazi zilizokuwa zimebaki zilikuwa ni kujenga jengo la utawala, kujenga maabara na kununua mashine maalum za kupigia shoti mnyama kabla hajachinjwa na mashine za kuchinjia, kujenga uzio katika eneo la mradi na kujenga zizi la chuma kwa ajili ya kutunza ng’ombe .

“Lakini cha ajabu kati ya Sh bilioni 1.1 zilizokuja, imejenga ukuta ambao haujaisha wala hauna plasta, pia zimejenga jengo la utawala ambalo mpaka sasa halijaisha hii ni aibu sana.

“Hata zile mashine za kupigia shoti na mashine za kuchinjia hazipo wakati walikuwa wameshaingia makubaliano ya kupata mashine hizo, lakini hazionekani na hazipo na machinjio imefunguliwa.

“Sasa ujue siasa ilivyo mbaya ili waonekane wao wanafanya kazi vizuri kuliko Chadema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefungua machonjio ikiwa na mapungufu yote hayo ili kuikomoa Chadema.

“Machichio hiyo iliyofunguliwa na kuitwa ya kisasa haina tofauti na ile ya Isoka ya awali iliyokuwa ikitumika jambo ambalo halina tija kwa wanachii wa Iringa.

“Ifike kipindi tuache kufanya siasa kwenye miradi ya maendeleo wanaona kama wakifanya hadema watasifiwa na wananchi na kuonekana wanafanya kazi nzuri,” anasema.

Kwa upande wake mmoja wa wakazi wanaokaa jirani na machinjio hayo, Edson Masawe nasema kuwa machinjio hiyo imefunguliwa kabla ya kukamilika hali inayosababisha kutoa harufu kali kwenye chemba za mashimo ya machinjio hayo kwani hayajafunikwa.

“Tuache siasa kwenye maishaa ya watu, hii machinjio haijakamilika yani huwezi kukaa nje kutokana na harufu kali inayotoka pale yani mpaka makonda wa daladala wakifika karibu na eneo hili huwataarifu abiria wao ‘sasa tunaingia kwenye eneo lenye harufu kali’ kwenye hili wanapaswa kukamilisha ili watu tukae kwa starehe sio unakaa ndani hata kula huwezi,” anasema Masawe.

Manispaa ya Iringa inajumla ya wakazi 152,345 kwa mujibuwa wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 watakaopata nyama kwenye machinjia hiyo

Wastani wa siku wa mapato yatakayopatikana kwenye machinjio hayo kwa siku ni Sh 198,000.

Hata hivyo, machinjio hayo yanatarajia kuajiri zaidi ya watu 200 wakiwemo wachinjaji, wachuna ngozi, wanaofanya usafi ndani na nje ya machinjio, wasafirishaji mifugo inayoletwa machinjioni pamoja walinzi wa usiku na mchana watakaolinda machinjio hayo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles