24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara yafaidika na matumizi ya Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara ni mojawapo ya taasisi zinazotumia nishati ya gesi asilia kwa kupikia mkoani Mtwara na imefurahia manufaa makubwa kutoka kwa nishati hiyo. Matumizi ya gesi asilia yameokoa pesa nyingi na kusaidia kutunza mazingira ya shule kuwa safi wakati wote. Aidha, ratiba za shule sasa zinaenda vizuri kwani chakula kinapikwa na kuiva kwa wakati.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC walipotembelea nyumba zinazotumia gesi asilia katika Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara, Juni 13, 2024.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) walipotembelea shule hiyo leo Juni 13, 2024. Akizungumza katika ziara hiyo, Makamu Mkuu wa shule, Mwalimu Bwire Babi, amesema, “Kabla ya matumizi ya gesi asilia, shule ilikuwa inatumia milioni sita hadi saba kila mwezi kwa ajili ya kununua kuni na mkaa. Lakini tangu kuanza kutumia gesi asilia mwaka 2020, kwa mwezi shule inatumia kiasi cha Sh 1,500,000 hadi 1,600,000. Tumepata unafuu mkubwa na tunashukuru Serikali na TPDC kwa kuleta gesi hii,” amesema Mwalimu Bwire.

Mwalimu Bwire ameongeza kuwa nyumba za walimu 31 shuleni hapo nazo zimeunganishwa na mtandao wa gesi asilia kwa matumizi ya kupikia, hali inayowaletea unafuu mkubwa wa nishati.

“Nilikuwa natumia hadi Sh 190,000 kwa ajili ya mkaa na gesi ya mitungi kupikia nyumbani kwangu, lakini sasa natumia Sh 30,000 tu kwa mwezi,” ameongeza Mwalimu Bwire.

Kwa upande wake, Mhandisi Samweli Charles, ameeleza kazi kubwa inayofanywa na TPDC katika kuunganisha Mtwara na mtandao wa gesi asilia kwa matumizi ya viwandani, majumbani, na kwenye taasisi.

“Hadi sasa, nyumba 425 zimeunganishwa na mtandao wa gesi asilia ya kupikia, pamoja na taasisi nne ambazo ni Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara, Chuo cha Ualimu Mtwara, Chuo cha Ualimu Ufundi Mtwara, Gereza la Lilungu na Kiwanda cha Saruji cha Dangote,” amesema Mhandisi Charles.

Makamu Mkuu wa Shule ya Ufundi Mtwara Mwl. Bwire akitoa ufafanuzi wa matumizi ya gesi asilia shuleni hapo kwa Wajumbe wa Bodi ya TPDC.

Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya TPDC imeonyesha jinsi gesi asilia inavyosaidia kuboresha maisha na kuleta unafuu wa gharama kwa watumiaji, na kuendelea kudhihirisha umuhimu wa nishati hiyo katika maendeleo ya jamii na uchumi wa Mtwara.

Makamu Mkuu wa Shule ya Ufundi Mtwara Mwl. Bwire akitoa ufafanuzi wa matumizi ya gesi asilia shuleni hapo kwa Wajumbe wa Bodi ya TPDC.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles