Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Shule ya Awali na Msingi ya Brookside iliyoko Kimara Suka, Wilaya ya Ubungo, Mkoa wa Dare es Salaam imeshika nafasi ya kumi ki- Mkoa na kuahidi kufanya makubwa zaidi.
Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Shule hiyo, Masanja Maduhu anasema kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha kwamba ndani ya miaka michache ijayo shule yao inakuwa kinara miongoni mwa shule za Mkoa wa Dar es Salaam.
“Tumejipanga na nina wahakikishia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwamba tutaendelea kifanya vizuri na wazazi waendelee kutuamini na kuleta watoto wao kwenye shule yetu,” anasema Maduhu.
Katika matokeo ya mwaka huu ya Darasa la Saba kwa mwaka 2023 Brookside imeshika nafasi ya kwanza katika Kata ya Saranga, nafasi ya pili katika Manispaa ya Ubungo na nafasi ya 10 Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya wazazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameipongeza shule hiyo kwa kutoa elimu bora na hatimaye kufanya vizuri Kimkoa.
“Kwa kweli naipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri na kulisaidia taifa kutoa elimu bora, anasema Magesa Bwire Mkazi wa Kata ya Ukonga, Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Masanja anasema kuwa siri kubwa ya mafanikio ya shule yao ni ushirikiano baina ya wadau wote wa shule Wazazi, Waalimu na uongozi bora.